Language

Friday, 12 April 2013

WATOTO HAWARUHUSIWI KUTAZAMA 'LOVE&POWER' YA KANUMBA



Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania, imeagiza kuwa filamu ya marehemu Steven Kanumba 'Love&Power'  inayotarajiwa kuingia sokoni rasmi leo, inatakiwa kuangalia na watu wenye umri wa kuanzia miaka 16 na kuendelea.
 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisoo aliagiza umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16 na kuendelea.
"Baada ya kuikagua filamu hii tumependekeza umri stahiki wa kutazama filamu hii ambao ni kuanzia umri wa miaka 16," alisema Fisoo.
Akizungumza Msemaji wa filamu hiyo Myovela Mfwaisa alisema Love&Power ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Tanzania.
"Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’. "
“Filamu ya Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety
‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na marehemu na kuongozwa na Steven Kanumba."
Alisema watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd na pia imetengenezwa  jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti tofauti.
 Myovela aliwaomba wasanii kuwa walinzi wa kazi hiyo ya marehemu kwa kupambana na maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu.
 "Tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua filamu ya Love & Power halali." alisema Myovela.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...