Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
safi na Maji taka Arusha, Injinia Ruthi Koya alisema kupatikana kwa kiasi hicho
cha fedha ndiko kutatatua tatizo la maji.
Alisema mamlaka hiyo haina kiasi hicho cha fedha kwa sasa bali
inategemea ruzuku ama mkopo ili kuweza kumudu kutatua tatizo la maji linalozidi
kulikabili jiji hilo, hasa baada ya kuongezewa maeneo kutoka wilayani Arumeru.
Injinia Koya alitaja maeneo ambayo hadi sasa hali ya upatikanaji maji
si nzuri ni pamoja na Olasity, Kwa Mrombo, FFU na baadhi ya maeneo ya Mianzini
ambapo jitihada zinafanywa kupunguza makali hayo.
Alifafanua kuwa baada ya mamlaka hiyo kuchimba kisima kirefu katika
eneo la Sombetini, wanatarajia kuyasambaza maji hayo katika maeneo ya Olasity
na Kwa Mrombo ambako kuna tabu kubwa ya maji.
Alisema uwezo wa mamlaka hiyo kwa sasa ni kuzalisha lita za ujazo
milioni 45,000 kwa siku huku mahitaji halisi yanayotakiwa ni lita milioni
93,270 kwa siku hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kufikia malengo hayo.
Aliomba wananchi kumvumilia kwa kipindi cha miaka mitano kuweza kutatua
changamoto hiyo ya upatikanaji maji safi na huduma ya uondoaji maji taka mjini
No comments:
Post a Comment