Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon ameitaka Korea ya kaskazini
kupunguza makali yake kwa mzozo unaotokkota wa kinuklia akisema kuwa umeanza
kuvuka mpaka.
Bwana Ban amesema kuwa anahuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia
maisha ya wananchi wa kawaida.
Akizungumzia vitisho vya karibuni sana vya Korea Kaskazini kwa Korea
Kusini na Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alisema kuwa
hali hiyo imekuwa ya kustajabisha na kusikitisha.
Alisema kuwa Korea Kaskazini imezidisha vitisho vyake na akaonya kuwa
cho chote kinaweza kuzusha kitendo cha kusikitisha.
Bwana Ban aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja
wa Mataifa, alitoa wito kwa viongozi wa Korea kaskazini kubadili mwenendo wao.
Awali msemaji wa Wizara ya mashauri ya Kigeni wa Urusi alisema kuwa
uamuzi wa Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa kuimarisha uwezo wake wa
zana za kinukilia unavuruga mipango ya kuanzisha upya mashauriano yanayohusu
mataifa sita ya kupatanisha Korea Kusini na Kaskazini.
Mataifa yanayokusudiwa kushiriki katika mashauriano hayo ni Korea
Kusini, Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Japan na Marekani.
Msemaji huyo alieleza kwamba juhudi zo zote za kupuuza maazimio ya
Umoja wa Mataifa hazikubaliki.
No comments:
Post a Comment