Language

Sunday, 14 April 2013

ANGALIA SANAA YA WATOTO HAWA


HIKI NDICHO ALICHOKIPOST MASANJA MKANDAMIZAJI KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK LEO


WAASI WA M23 WATOA ONYO KWA TANZANIA

Waasi wa kundi la M23 wameitaka Tanzania kuachana na mipango ya kuchangia wanajeshi wake katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopangwa kutumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kupambana na waasi .
Waasi wa kundi hilo la M23 ambao wamekanusha madai ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwamba nchi jirani za Rwanda na Uganda zinawaunga mkono,wameonya katika baruwa iliyotumwa na kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo Betrand Bisimwa kwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kwamba daima wamekuwa wakipata ushindi dhidi ya vikosi vikubwa vyenye silaha nzuri.
Bisimwa ameandika " Jambo kama hilo litawakuta kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa cha kuingilia kati iwapo busara yao itashindwa kufanya kazi kuingilia kati na kuzuwiya hali ya hatari ilioko kwenye mkondo huo."
Bisimwa amesema kwa ajili hiyo kundi hilo la waasi la M23 linaomba bunge na wananchi wa Tanzania kufikiria upya kwa uangalifu juu ya hali hiyo na kuishawishi serikali ya Tanzania kutowapeleka watoto wao wa kiume na wa kike wa taifa hilo la uadilifu kushiriki kwenye vita vya kipuuzi dhidi ya ndugu zao wa Congo.

ALIYEKUFA NA KUZIKWA GEITA MIAKA 5 ILIYOPITA AFUFUKA



Mji wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa.

Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.
“Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,”alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.
Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: SHILINGI BILIONI 620 ZA DENI LA TAIFA HAZINA MAELEZO



 


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa
sana katika akaunti ya Deni la Taifa. Nanukuu

‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30
Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi
619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.’
(Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158). Mwisho wa Kunukuu.

Katika Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha
kuwa Deni la Taifa linazidi kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni
lilikuwa kwa asilimia 17 kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.
Kukosekana kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi

AUNT EZEKIEL AMLILIA KANUMBA KABURINI PEKE YAKE!!!



STAA kiwango wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amenaswa kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba peke yake baada ya watu wote kuondoka.

Tukio hilo lilitokea juzikati katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo tofauti na wasanii wengine waliofika kumuenzi marehemu aliyekuwa akitimiza mwaka mmoja kaburini, Aunt alibaki peke yake, akapiga magoti kaburini na kuanza kulia kwa uchungu.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika makaburi hayo, walishangazwa na tukio la Aunt kukaa makaburini kwa takribani dakika kumi huku wengine wakimuonea huruma kutokana na msanii huyo kushindwa kuzuia hisia zake.
“Kiukweli kila nikifika katika kaburi la Kanumba lazima nihisi kuchanganyikiwa. Kuna wakati mwingine siamini kabisa kama huyu mtu hatunaye tena hivyo nahitaji kubaki hata peke yangu kaburini nimsalie kisha niondoke,” alisema Aunt huku akifuta machozi.

AJALI YA GHOROFA ILIYOUA 36, MSANII WA BONGO FLAVA PIA ALIKUFA



WAKATI Watanzania wakianza kusahau msiba wa kuanguka kwa jengo lenye ghorofa 16 Machi 29, mwaka huu jijini Dar, imegundulika kati ya watu 36 waliofariki dunia kutokana na ajali hiyo, yumo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Gabriel Godwin Kimwela.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Mboka Godwin, Gabriel alikuwa akifanya shughuli za ujenzi katika jengo hilo  lililopo kati ya Mtaa wa Indira Ghandhi na Barabara ya Morogoro na alifariki mara baada ya jengo hilo kuanguka.
“Maiti tuliisafirisha na kuipeleka Mbeya,” alisema Mboka na kuongeza kuwa mbali na kuwa msanii, kaka yake aliwahi kujihusisha na siasa kwa kuwapigia debe wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na John Mnyika katika Kampeni za Uchaguzi  Mkuu wa mwaka 2010.
Katika sanaa, Gabriel aliwahi kutoa albamu moja kwa ufadhili wa shirika moja la Kimarekani iliyorekodiwa katika ya Zinji Record.
Nyimbo zake zilizopata kusikika redioni ni Africulture na Tumeshachoka. Mwaka 2004, Gabriel alianzisha Kundi la Wakubwa Family ambalo baadhi ya wasanii wake  wanajipanga  kumtungia wimbo wa kumuenzi wakimshirikisha Z-Anto.

YUSUPH MLELA AMDUNGA MIMBA MWANAFUNZI



Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.

 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.
“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo  anachosoma hakijui.
“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko,  kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.

MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA JANA


BODY PARTY LYRICS-CIARA



"Body Party"
My body is your party, baby
Nobody's invited but you baby
I can do it slow now, tell me what you want
Baby put your phone down, you should turn it off
Cause tonight is going down, tell your boys is going down
We in the zone now, don't stop
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...