Language

Wednesday 23 January 2013

HABARI: HAYA NDIO MATOKEO YA UCHAGUZI ISRAEL

Wapiga kura wa Israel wamemuondowa patupu waziri mkuu Netanyahu anaekabiliwa na kazi ngumu kuweza kuunda serikali ya muungano 

Waisraeli wamepiga kura jana, na wamezusha maajabu. Mtangazaji wa zamani wa televisheni, Jair Lapid na chama chake cha kiliberali - Yesh Atid - amemaliza nafasi ya pili akijikingia viti 19 vya bunge la Knesset. Yeye ndiye mshindi mkubwa wa uchaguzi huo. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameondolewa patupu na wapiga kura. Muungano wa vyama vya mrengo wa kulia vya Likud na Beitenu, anaouongoza, umejipatia viti 31 toka jumla ya viti 120 vya bunge la Israel - Knesset.
Baada ya ushindi kama huo, kimsingi mshindi hupanda ndani ya gari la fakhari
. Yair Lapid lakini hakutaka makubwa na badala yake ameamua kupanda teksi kutoka nyumbani kwake kwenda katika ukumbi wa sherehe zilizoandaliwa na chama chake.Mshindi halisi wa uchaguzi huo Yair Lapid anasema:"Taifa la Israel linakabiliwa na changamoto kubwa. Inabanwa na mgogoro wa kiuchumi ambao ni kitisho kwa watu wa tabaka la wastani. Israel inakumbwa na kitisho cha kutengwa kimataifa. Njia ni moja tu kuweza kuzishinda changamoto hizo; Ushirikiano na mshikamano."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...