Language

Tuesday 29 January 2013

MICHEZO: DROGBA KUICHEZEA GALATASARAY KWA MWAKA MMOJA NA NUSU


Galatasaray imemsajili aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba kutoka kwa klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki katika ligi kuu ya Premier nchini Uchina.

Galatasaray inayocheza ligi kuu nchini Uturuki, imethibitisha kuwa Drogba amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na klabu hiyo.
Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga barani ulaya kwa mara nyingine.
Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.
''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...