Language

Friday 8 February 2013

HABARI MUHIMU: MAPENZI YAUA MMOJA KILIMANJARO

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu kujinyonga kwa kutumia kipande cha kanga.
Katika tukio la kwanza mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Aloyce Msabaha (58), mkazi wa Kibosho Kitandu, Moshi Vijijini alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kanga na kuacha ujumbe mzito kuhusiana na kifo chake.
Shuhuda wa tukio hilo, aliyefahamika kwa jina la Msabaha ambaye ni baba wa familia ya mke na watoto haifahamiki ilikuwaje mpaka akafikia hatua ya kusitisha uhai wake japo taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai ni wivu wa mapenzi.
Hata hivyo Shuhuda huyo  amesema waulikuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia katika mti wa mwembe uani, nyumbani kwake.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amesema, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, polisi walifika katika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu pamoja na karatasi kilichokuwa na ujumbe.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa saba usiku ambapo inadaiwa kuwa mwili wa marehemu uligundulika asubuhi ukiwa umening’inia katika mti wa mwembe jirani na nyumba ya marehemu.
Katika tukio la pili, Mtembea kwa miguu, Raphael Maro (48), mkazi wa Uru Kariwa aligongwa na pikipiki, lililokuwa likiendeshwa na mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja kutokana na kukimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Kamanda Boaz amesema tukio hilo lilitokea, Februari 5, majira ya saa 4 usiku, katika barabara ya Uru eneo la makelele na kuongeza kuwa Jeshi lake linamsaka mtu huyo kutokana na kutoroka baada ya kusababisha kifo cha mwenda kwa miguu ambaye alikufa papohapo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...