Language

Wednesday 27 February 2013

HABARI MUHIMU: PAPA BANEDICT WA 16 AAGWA NA WAUMINI ROMA

Waumini kutoka Bavaria,wakishirikiana na wenzao kutoka kila pembe ya dunia wamuaga kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni
Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Papa Benedikt wa 16 atakaestaafu kuanzia february 28 na kujishughulisha zaidi na ibada na kutafakari,anaongoza misa yake ya mwisho katika uwanja wa Mtakatifu Petro,wakihudhuria zaidi ya waumini laki moja na nusu kutoka kila pembe ya dunia.Wakaazi wa jimbo la kusini mwa Ujerumani Bavaria anakotokea kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni wamekuja kwa wingi kumuwaga jamaa yao.
Katika misa yake hiyo ya mwisho ya hadhara kama kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,Papa Benedikt wa 16 akiwa ndani ya gari maalum la Vatikan anawaamkia umati wa waumini waliojazana katika uwanja wa Mtakatifu Petro,muda mrefu zaidi kuliko kawaida yake kabla ya kuwakaribisha kwa mazungumzo baadhi ya
viongozi ikiwa ni pamoja na rais Ivan Gasparovic wa jamhuri ya Slovakia.
Miongoni mwa waumini hao kuna wale wanaotokea katika jimbo la kusini la Bavaria,wakibeba bendera za jimbo hilo na kupiga muziki wa Bavaria ambao mwenyewe Joseph Ratzinger anapenda kuusikia uklichezwa.
Tangu siku kadhaa zilizopita,umati wa waumini kutoka Ujerumani wamekuwa wakimiminika mjini Roma.Wenyewe wanasema hata akiacha wadhifa huo kesho february 28,ataendelea kuwa muhimu kwao.
Tobias Eichinger aliyekuja Roma pamoja na mchumba wake Cornelia anasema:"Tunataka kumuombea Papa mtakatifu ambae ni wa kutoka Bavaria na pia ni mwenzetu, kila la kheri .
Tobias Eichinger anasema ingekuwa vyema Joseph Ratzinger, atakapostaafu,kama kwa mfano atamtembelea kakaake Georg anaeishi katika eneo la Regensburg.Hilo litawafurahisha maelfu ya waumini wa kikatoliki na sio mie peke yangu anasema na kuungama wakati huo huo kutokana na sababu za usalama jambo hilo pengine halitowezekana

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...