Language

Saturday 9 February 2013

MICHEZO: HIVI NDIVYO DROGBA ALIVYO POKELEWA UTURUKI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba amepata mapokezi mazuri alipowasili Istanbul alipokubali kujiunga na Galatasaray ya Uturuki katika uhamisho wa Januari.

Kiungo wa zamani wa Inter Milan, Wesley Sneijder alipata mapokezi kama hayo alipowasili Uturuki mwezi uliopita na Drogba ameamua kumfuata Mholanzi huyo akiondoka Shanghai Shenhua ya China.
Nahodha huyo wa Ivory Coast alichelewa kuwasili kwenye timu hiyo kwa sababu ya Fainali za Mataifa ya Afrika.
Drogba ataungana na Emmanuel Eboue, ambaye alijiunga na klabu hiyo bingwa ya Uturuki akitokea Arsenal mwaka 2011.
Mshambuliaji mwingine wa zamani wa Chelsea, ambaye alitoka Stamford Bridge kwenda China, Nicolas Anelka amerejea Ulaya. 
Nicolas Anelka alijiunga na Shenhua Januari mwaka jana, lakini ameamua kujiunga na vigogo wa Italia, Juventus, akikamilisha uhamisho wake kwa mabingwa hao wa Serie A mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...