Language

Monday 11 March 2013

HABARI MUHIMU: MWANAJESHI AUA WATU 9 BAA



Mwanajeshi mmoja nchini Uganda anadaiwa kuwapiga risasi na kuwauwa watu 11 wakiwemo wenzake watatu baada ya mzozo katika baa moja nchini humo.

Polisi walisema wanamsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambayo yalitokea katika maeneo mawili tofauti juzi, huko Entebbe kwenye Wilaya ya Wakiso na kambi ya jeshi ya Bombo iliyopo kwenye Wilaya ya Luweero.

Polisi imesema kisa hicho kimetokea katika baa iliyoko kwenye soko moja mjini Bombo kilomita 30 kutoka mji mkuu Kampala, ambapo watu 10 waliuawa papo hapo huku mmiliki wa baa hiyo ijulikanayo kama Four Turkeys akipigwa risasi kwenye lango la kuingilia na baadaye kufariki dunia akiwa hospitali.
Akizungumza na mjini Kampala, naibu msemaji wa Polisi wa Uganda, Judith Nabakooba, alithibitisha kisa hicho na kusema kwamba kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kujua sababu ya mauaji hayo. Nabakooba alisema huenda hali hiyo ikawa imechochewa na kutoelewana.
“Wataalamu wetu wanatafuta silaha iliyotumika katika mauaji hayo na baada ya kuipata ndipo tutakapopata mwanga kuhusu muuaji,” alisema.
Wakazi wa eneo hilo walisema kwamba mtu huyo anayedhaniwa kuwa ni askari aliingia katika baa hiyo wakati kiza kilipoanza kuingia na kufyatua risasi mfululizo kisha kutoweka.
Hata hivyo, visa vya mauaji kama haya vinavyowahusisha wanajeshi na polisi walevi si vigeni nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...