Language

Friday 1 March 2013

HABARI MUHIMU: KONDOM FEKI ZINAZIDI KUSAMBAZA MAAMBUKIZI YA HIV/AIDS


WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku  Uingereza mwaka jana zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za gonjwa la ngono hatari lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25 Uingereza, huku wataalamu wakionya kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye vipele vipele ambazo mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza iliingia katika msako mkali  kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi 18 iliyopita.

Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari kimetajwa kuwa ni 'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu ya  viuavijasumu (antibiotics) ambayo angalau hufanya kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu hizo nchini , Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri Kinabo  alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na Dawa(TFDA) hivi sasa lipo katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi vya ubora wa bidhaa hizo vinaangaliwa.
"Hili suala ni nyeti na ni la kiafya na usalama zaidi, hivyo tulikaa kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa kondom hizi, kwani ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora linatakiwa kuangaliwa," alisema Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili waweze kuchunguza bidhaa hizo kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili  kutaka kujua uhalali wa bidhaa hizo sokoni, Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini hupimwa, lakini kuna baadhi ya bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo halali na mara nyingi huwa feki.
"Inetegemea na lebo ya bidhaa husika, kuna wakati bidhaa inaweza kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa sokoni, lakini baada ya muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo, hivyo hilo ni suala la kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa kuanzishwa kwa kampeni mpya ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa hayo nchini Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa kusambaa kwa wingi nchini humo na nchi zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada ya kuanzishwa mpango mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea Resistance Action Plan' ambayo itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi wa Afya, utafuatilia tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu kupungua miaka 10 iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...