Language

Friday 1 March 2013

MICHEZO: BENITEZ OUT MEI MWAKA HUU


Rafael Benitez, amesema kuwa atakihama klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.

Akiongea baada ya kuongoza Chelsea kushinda klabu ya Middlesbrough kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya raundi ya tano ya kuwania kombe la FA, kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile aliwashutu mashabiki wa klabu hiyo.
Katika mahojiano na BBC, Benitez amesema uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha
kaimu kocha wa klabu hiyo ilikuwa kosa kwa sababu yeye ndiye kocha mkuu kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa msaada wanaohitaji na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.'' Mashabiki sasa hawana sababu ya kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Mashabiki wa Chelsea wakiwa na mabango ya kumtaka kocha huyo kufutwa kaziTangazo hilo la kocha huyo wa zamani wa Liverpool limejiri baada ya baadhi ya mashabiki wa klabu huyo kumdhihaki baada ya mechi yao na Middlesborough.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, hajapata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo tangu alipoteuliwa kuchukua mahala pa Roberto Di Matteo mwezi Novemba mwaka uliopita.
Katika mechi nyingi zilizopita za Chelsea, mashabiki wa klabu hiyo hawakuficha hisia zao za kutaka kocha huyo kufutwa kazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...