Language

Friday 1 March 2013

BURUDANI: LADY JAY DEE KULETA JOTO NA HASIRA

MWANAMUZIKI wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo au Lady Jay Dee, yuko kwenye matayarisho ya albamu yake ya sita, na tayari ameshatengeneza nyimbo mbili, mmoja akiwa amefanya mwenyewe na wa pili akiwa amemshirikisha Profesa Jay, wimbo unaoitwa Joto na Hasira.

  
Jay Dee ambaye pia ni mmiliki wa mgahawa wa Nyumbani Lounge, ameliambia gazeti hili kwamba ujio wake wa safari hii utakuwa wenye ubunifu wa hali ya juu, kutokana na kile anachosema kwamba ana uzoefu zaidi kuliko ilivyo awali na pia anataka kuzikonga nyoyo za wapenzi wake.
Maendeleo ya utengenezwaji wa albamu hiyo yanavyoendelea yatakuwa yakionyeshwa katika kipindi chake cha Diary ya Lady Jay Dee kinachoonyeshwa na kituo cha Televisheni cha EATV.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...