Language

Saturday 30 March 2013

PROFESA JAY HASHANGAI MAFANIKIO YAKE

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule, a.k.a Profesa Jay, amesema hajashangaa kujikuta katika orodha ya mwanzoni kabisa ya wanamuziki wa heshima waliotajwa kushiriki tamasha lililoandaliwa na mwanamuziki nguli kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone.

Jay ambaye kwa mujibu wa Chameleone mwenyewe, ataambatana na mwanamuziki mwingine aliyewahi kuwika na miondoko ya Takeu, Lucas Mkenda, au Mr Nice, amesema heshima kama hizi haziji hivi hivi ila zinatokana na kuhangaika kwake na muziki huu wa kizazi kipya na kuhakikisha kwa kila njia unafika katika hatua nyingine.
Katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na Mwananchi, Jay amesema ukiachana na suala la muziki, yeye ni kama kaka wa wanamuziki kwa sasa.
Jay ambaye kwa sasa anasikika katika vituo vingi vya redio kupitia nyimbo zake nyingi ukiwamo ule alioshirikishwa na Lady Jaydee wa Joto na Hasira, anatajwa kuwa mwanamuziki aliyetia ushawishi wa hali ya juu kwa wasanii wachanga kuanza muziki hapa nchini.
Onyesho hilo linatarajia pia kukusanya na wanamuziki kutoka Kenya, litafanyika katika siku tatu mfululizo ambapo siku ya kwanza, itakuwa ni tarehe 26 Aprili, katika viwanja vya mchezo wa rugby vya Kyandondo jijini Kampala, kisha Colline Hotel siku itakayofuata katika Mkoa wa Mukono na litafunwa Entebe tarehe 28 katika fukwe za rResort Beach.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...