Language

Saturday 30 March 2013

HALI YA NELSON MANDELA INAENDELEA KUIMARIKA


Maafisa wa utawala nchini Afrika Kusini wanasema kuwa rais mstaafu Nelson Mandela anaendelea vyema na matibabu baada ya kulazwa hospitalini kwa siku ya pili akiwa na maradhi ya kifua.


Taarifa kutoka rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ilisema kuwa hali ya Mandela inaendelea kuimarika na kwamba hata aliweza kula vyema kiamsha kinywa chake.
Mapema leo Jacob Zuma, aliwahakikishia wananchi wa Afrika Kusini kuwa rais mstaafu Nelson Mandela anatibiwa ugonjwa wa mapafu ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara.
Katika mahojiano na BBC , bwana Zuma alisema kuwa watu hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani Mandela anaendelea kupokea matibabu.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kabla ya Jumatano usiku.
Alikuwa hospitalini kwa siku 18 mnamo mwezi Disemba, akipokea matibabu ya mapafu na kibofu.
Katika taarifa yake iliyotolewa mapema, Zuma alisema kuwa Mandela anaendelea kupokea matibabu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...