Language

Thursday 4 April 2013

7 WAPOTEZA MAISHA DAR ES SALAAM KATIKA MATUKIO TOFAUTI



Watu  wawili wamekufa maji na wengine idadi kama hiyo, kukijeruhiwa  katika matukio tofauti  yaliyotokea jijini Dar es Salaam.   

Kamanda wa Mkoa wa  Kipolisi  wa Kionondoni, Charles Kenyela ,alisema katika mkoa huo,   maiti ya mtu mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Magreth Kusupa (35), imekutwa ikiwa inaelea juu ya maji katika Mto Mbezi.
Alisema maiti huyo alikutwa saa 2:00 asubuhi  katika eneo la Goba na kwamba wananchi wa eneo hilo, walifanya jitihada za kumopoa.
Alisema “Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mwili wa marehemu  haukuwa na jeraha na umehifadhiwa  katika Hospitali ya Mwananyamala.”Kamanda  Kenyela alisema mtu mwingine aliyetambuliwa kuwa ni Serafini Ameros,  mpiga tofali amekufa maji na wenzake wawili, wakiwa wamejeruhiwa wakati wakijaribu kuokoana kwenye karo lililojaa maji.
Kamanda Kenyela alisema tukio hilo lilitokea saa 8:00 mchana  katika eneo la Mbezi Msakuzi  wakati  Amaros akijaribu kuondoa uchafu kwenye shimo ambalo lingetumika kama choo.
Alisema shimo hilo liko nyumbani kwa Damian Laurent  ambaye katika tukio hilo alijeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...