Language

Saturday 27 April 2013

JUSTIN BIEBER HANA MSIMAMO KWA WANAWAKE, KAMBWAGA JASMIN VILLEGAS NA KUMRUDIA SELENA GOMEZ

Baada ya tetesi na ushahidi mwingi niliowahi kukupatia kupitia hapahapa BONMUSIC BLOG kuhusu Justin Bieber kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Selena Gomez na kumuacha njia panda Jasmine Villegas ambaye ndiye mpenzi wake mpya, sasa Justine ametuma Hot picture katika Instagram, picha inayoashiria kila dalili ya mapenzi mazito kati yao.

Na kama picha ya  Justin Bieber na Selena Gomez haitoshi kuelezea kilichopo kati yao kwa sasa, maandishi yaliyo chini ya picha hiyo (caption) yameandikwa “umetengeneza muziki kwa muda mrefu mpenzi, njoo unikumbatie”…ni dhahiri kuwa maneno hayo yameandikwa na Selena Gomez. 

Jasmine Villegas
Pamoja na hilo, Beliebers na Seleantors wanazunguka pande mbali mbali za dunia pamoja wakisherehekea kwa kilichotokea  ni official confirmation kuwa wawili hao wako katika dimbwi la mapenzi tena.
 
Ni wazi kuwa Justin ameamua kuliweka penzi lake hadharani kwani wiki iliyopita pia nilikiujuza kupitia hapahapa na kukuonesha picha iliyowaonesha wawili hao wakikiss wakati Justin akiwa back stage.

Justin na Selena kupiga na kuweka picha nyingine za kimahaba? Katika picha hiyo Selena pia hakuwa na shirt kama Justin? Where are her hands positioned? Na nini kilifuata baada ya hiyo picha kupigwa?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...