Language

Saturday, 16 March 2013

HABARI MUHIMU: KENYATTA APATA MTIHANI WA KWANZA, BEI YA MAFUTA IMEPANDA KENYA

Tume ya Nishati  imetangaza ongezeko la bei ya petroli kwa Sh4.12 na kuibua hofu kwamba huenda kiwango cha mfumuko kikapanda tena.

Hii ni mara ya pili kwa bei kupanda baada ya kushuka kwa muda. Petroli sasa itauzwa Sh117.69 kwa lita Nairobi.
Bei ya dizeli ilipanda kwa Sh1.17 hadi Sh107.37 kila lita jijini, nayo mafuta taa yakapanda bei kwa Sh2.61 hadi Sh88.54 kwa lita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa ERC Kaburu Mwirichia ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la kimataifa.
Bei ya mafutaghafi ilipanda kwa asilimia 3 kwa pipa hadi Dola 115 Februari kutoka Dola 112.05 kwa pipa Januari mwaka huu.
Bei ya mafuta taa yaliyosafishwa iliongezeka kwa asilimia 8.15 kipindi hicho, nayo ya petrol ikapanda jwa asilimia 5.68 na ya dizeli asilimia 3.38.
“Katika kipindi hicho kiwango cha ubadilishanaji wa shilingi ya Kenya na Dola ya Amerika kilibaki thabiti kiasi katika Sh87.31 Februari ikilinganishwa na Sh87.01 Janauri,” alisema Mwirichia.
Mwezi uliopita, bei ya petrol ilipandwa kwa Sh1.97 kwa lita, dizeli kwa Sh2.21 kwa lita na mafuta taa kwa Sh2.07.
Mwezi huo, kiwango cha mfumuko kilipanda kwa mwezi wa pili mfululizo hadi 4.45 kutoka asilimia 3.67 Januari baada ya kushuka kwa miezi 13.
Hali huenda ikawa mbaya kutokana na uhaba wa vyakula ambao unasababisha kupanda kwa bei za vyakula.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...