Papa Francis I aliteuliwa hivi karibuni kuliongoza kanisa hilo baada ya
Papa Benedict XVI kutangaza kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Enzi ya ujana wake aliwahi kufanya kazi mbalimbali ikiwamo ya mlinzi wa
mlangoni (baunsa) katika Bar, ili kujipatia fedha.
Papa Francis aliteuliwa hivi karibuni kuliongoza kanisa hilo baada ya
Papa Benedict XVI kutangaza kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Aidha, Papa Francis anatarajia kuongoza misa yake ya kwanza kesho
katika Kanisa la Mtakatifu Peter, mjini Vatican.
Katika wasifu wake ulioandikwa mwaka 2010 na Francesca Ambrogetti na
Sergio Rubin wa Shirika la Jesuit, Papa Francis I alikiri kuwa aliwahi kufanya
kazi kama mlinzi wa mlangoni katika moja ya baa za Jimbo la Buenos, Argentina,
ili kujipatia ada ya shule.
Papa huyu mpya ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio,
alisema kuwa rafiki yake wa kike alikuwa ni miongoni mwa kundi la marafiki
aliokuwa akicheza nao muziki wa tango.
“Lakini baada ya kubaini kuwa natakiwa kuenenda kiroho, nilisitisha
urafiki,” alisema alipohojiwa.
Papa Francis I amezaliwa katika familia yenye maisha ya kawaida, ambapo
baba yake alikuwa mfanyakazi wa shirika la reli na mama yake alikuwa mama wa
nyumbani.
Vilevile kuna taarifa zinaeleza kuwa Papa Francis, aliwahi kumpenda
msichana mmoja na kutaka kuoa kabla ya kuingia katika utumishi wa Mungu.
Mwanamke huyo Amalia Damonte alisema kuwa aliwahi kutaka kuolewa na
Papa, lakini alikataa.
“Nampa hongera Papa Francis, lakini nilikataa ombi lake la kutaka
kunioa,” alisema Damonte.
Alisema Bergoglio alionyesha nia ya kumwoa akiwa na miaka 12 na
alikataa kwa sababu wazazi wake wasingekubali akiwa katika umri huo.
No comments:
Post a Comment