Zaidi ya mashirika 12 ya kutetea haki za binadamu na
haki za wanawake kutoka mataifa ya kiarabu yameonya kuwa azimio la UN la
kukabili unyanyasaji wa wanawake linatishiwa na upinzani kutoka kwa
chama cha Muslim Brotherhood kutoka Misri, uongozi wa Vatican na Urusi.
Azimio hilo liko katika hatua za mwisho za
mashauriano kabla ya kuidhinishwa na tume ya kutetea maslahi ya wanawake
katika Umoja huo.
Muslim Brtoher hood imesema kuwa azimio hilo
linatishia kuvuruga mpangilio katika jamii kwa kuwapa wanawake ruhusa ya
kusafiri, kufanya kazi au hata kupanga uzazi bila idhini ya waume wao.
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu
kutoka mataifa ya arabuni (hasa Misri, Lebanon Palestine, Jordan na
Tunisia) yametoa wito kwa mataifa yaliyo na uakilishi katika tume hiyo
ya UN juu ya haki za wanawake, yakome kutumia dini, utamaduni na mila
kama kisingizio cha kuruhusu ukiukaji wa haki na unyanyasaji wa
wanawake.
No comments:
Post a Comment