Msanii wa bongofleva Timbulo amesema kuwa yeye si msanii ambaye amepata
umaarufu kutokana na skendo kuliko kazi anayofanya ya muziki.
Timbulo amesema kuwa watu wanaosema kuwa yeye anapendwa kutengeneza
skendo ili aandikwe kwenye magazeti wanakosea kwa kuwa angetaka kufanya hivyo
basi angekuwa anatengeneza stori nzuri na si za kumchafua.
Msanii huyo alisema kuwa hajawahi kufanya kitu kama hicho kabisa,
"kuna vitu vya kutengeneza lakini si kashfa ambayo inaweza kuwa kidonda
cha milele, ningekuwa nataka kutengeneza kashfa nzuri basi ni bora
ningetengeneza stori za uwongo kuwa nimeenda kutoa msaaada sehemu flani lakini
si kwa kujichafua jina langu".
Tangu atoke na wimbo wa kwanza 'Domo langu' mwaka 2011 msanii huyo
amekuwa akiandikwa kwenye magazeti kwa skendo kuliko kazi anazofanya.
Hivi karibuni pia Timbulo aliwahi kuripotiwa kwamba amekamatwa na
madawa ya kulevya nchini burundi huku picha yake akiwa na madawa ikisambazwa
kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii na magazeti tando,n lakini siku chache
baadae, tukio hilo lilikanushwa.
Timbulo ambaye jina lake halisi ni Ally Timbulo aliongeza pia kuwa
alikuwa atoe wimbo wake wiki hii kabla ya Pasaka lakini kutokana na yeye kupata
onyesho la pasaka mkoani atashindwa kutoa wimbo wake mpya.
No comments:
Post a Comment