Language

Thursday, 28 March 2013

VIONGOZI WA DECI KUHUKUMIWA HIVI KARIBUNI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Mei 10, mwaka huu inatarajia kupanga siku ya hukumu ya  kesi  ya kuendesha na kusimamia mchezo wa upatu inayowakabili vigogo wa Taasisi ya Deci  Tanzania Ltd.

Hakimu Mkazi, Stuwart Sanga, jana   alizitaka upande zinazohusika katika kesi hiyo, kuwasilisha mahakamani hoja zao kama washtakiwa wana hatia ama la.
Alisema “hoja hizo zinapaswa kuwasilishwa Mei 10 na kwamba siku hiyo hiyo atapanga siku ya hukumu.”
Hatua hiyo imekuja baada ya vigogo wa Deci, kumaliza kutoa utetezi wao kuhusu  mashtaka mawili yanayowakabili.
Mashtaka hayo ni pamoja na kuendesha mradi wa upatu kinyume na sheria za taasisi za fedha na kuendesha mradi huo bila kibali.
Julai 17, mwaka jana mahakama hiyo, iliwaona washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu na kuwataka kujitetea  baada ya mashahidi 16 wa upande wa mashtaka, kutoa ushahidi wao.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya mwaka 2007 na  Machi 2009, washtakiwa walikuwa wanachukua amana za watu bila ya kibali.

Anadaiwa kuwa washtakiwa hao waliomba kibali cha kuendesha shughuli za kifedha na  si cha kuchukua amana kutoka kwa wananchi.
Inadaiwa kuwa zaidi ya Watanzania 700,000 kote nchini walijiunga na taasisi hiyo na walikuwa wakipanda na kuvuna pesa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...