Rais wa Marekani Barrack Obama, ametoa onyo jipya kwa Syria kwamba
matumizi ya silaha za maangamizi makubwa dhidi ya raia nchini humo huenda
likapelekea kubadilisha msimamo wa Marekani juu ya kuingilia kijeshi Syria.
Obama ametoa onyo hilo wakati akiwa anakabiliwa na shinikizo kutoka
nchini mwake na bara la ulaya kwa ujumla kuingilia mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe nchini Syria.
Hata hivyo siku moja baada ya Marekani kusema kwamba kemikali hizo
zenye sumu huenda zimetumika kwa kiwango kidogo, Obama anasema nchi yake lazima
iwe na uhakika wa matumizi ya silaha za kemikali, na ushahidi unaoonyesha
silaha hizo zimetumika kivipi na wapi.
" Tumeshawahi kuona picha mbaya sana zamani, baada ya maafisa wa
ulinzi wanaoonekana kufanya maamuzi kutokana na maswala ya sera, na baadaye
inakuja kubainika kuwa ushahidi iliopelekea maamuzi hayo kufanywa si wa ukweli
," alisema afisa mmoja wa ulinzi nchini Marekani ambaye hakutaka jina lake
litajwe.
Afisaa huyo alikuwa akitoa mfano wa namna Marekani ilivyoiingilia
kijeshi nchini Iraq baada ya kugundua kuwa silaha za maangamizi yenye nguvu
zinatumika katika ghasia za nchi hiyo madai ambayo baadaye yalisemekana sio ya
kweli. Katika ghasia hizo za mwaka 2003, wanajeshi 4,500 wa Marekani waliuwawa
huku raia wengi wa Iraq pia wakipoteza maisha yao.
No comments:
Post a Comment