Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelitangaza baraza lake la mawaziri ambalo
kwa kiasi kikubwa limeundwa na sura ngeni na wengi wao ni wasomi waliobobea
kwenye fani mbalimbali.
Katika majina 16 aliyopendekeza ambayo baadaye yatafanyiwa uchunguzi na
Bunge kabla ya kuidhinishwa, Rais Kenyatta amezirejesha sura mbili ambazo
zilizoeleka kwenye siasa za Kenya, ambao ni Najib Balala na Charity Ngilu.
Wote kwa pamoja walikosa ubunge katika majimbo yao kwenye uchaguzi wa
Machi 4, kutokana na kumuunga mkono Uhuru, lakini alisema kwamba amewaagiza
kuachana na siasa ili kutekeleza majukumu yao mapya.
Balala ambaye amependekezwa kuwa Waziri wa Madini, wakati Ngilu
akipendekezwa kuwa Waziri wa Nyumba na makazi, kunatazamiwa kuzusha mjadala
mkubwa miongoni mwa makundi ya kijamii.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Ulinzi, Rachel Omamo ni miongoni mwa uamuzi
unaozua mjadala kuhusu uwezo wa Serikali mpya ya Kenyatta kutokana na nchi hiyo
kukabiliwa na tishio kubwa la kiusalama hasa kutoka kwa wanamgambo wa
Al-Shabaab wa Somalia.
Akitangaza baraza hilo la mawaziri kwa kuwaita mmojammoja na kutaja
wasifu wao kisha kuwapa muda wa kuzungumza, Kenyatta alisema baraza lake
litakuwa la mawaziri wanataaluma na wanasiasa watakuwa wawili tu, yaani yeye na
makamu wake, Ruto.
“Tumekubaliana kwenye baraza letu kutakuwa na wanasiasa wawili tu, mimi
na Makamu wa Rais William Ruto,” alisema Rais Kenyatta mara baada ya kumaliza
kutangaza majina ya mawaziri hao Ikulu.
Awali Rais Kenyatta alitangaza majina manne likiwemo jina na
mwanadiplomasia wa siku nyingi ambaye hivi karibuni alianzisha kampeni ya
kuwania nafasi ya Ukurugenzi katika Shirika la Biashara Duniani (WTO), Amina
Mohammed.
Amina amependekezwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, akiwa ni mwanamke wa
kwanza kuteuliwa katika nafasi hiyo tangu Kenya ijinyakulie Uhuru wake mwaka wa
1963.
Mawaziri wengine waliopendekezwa ni Adan Mohamed ambaye kabla ya uteuzi
huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Baclays Afrika (Viwanda na
Maendeleo ya Biashara), Anne Waiguru (Maendeleo ya Wananchi na Mipango), na
Felix Tarus Kosgey (Kilimo, Mifugo na Uvuvi).
Wengine ni Judy Wahungu (Maji na Maliasili), Hassan Wario (Michezo na
Utamaduni), Jacob Kaimenyi (Elimu), Francis Kimemia (Katibu wa Baraza la
Mawaziri) na Lawrence Lenayapa (Mnadhimu wa Ikulu).
Waziri mwingine aliyeteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa katika baraza
lake la mawaziri ni Henry K. Rotich, kuongoza Wizara ya Fedha. Rotich ambaye ni
msomi na mchumi alifanya kazi kwa muda mrefu katika Wizara ya fedha nchini
Kenya na hata katika Benki Kuu ya nchi hiy
No comments:
Post a Comment