Language

Saturday, 6 April 2013

MIAKA 10 JELA KWA KUMNYONYA ULIMI MTOTO WA MIAKA 13



MAHAKAMA Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41) mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa yake.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni akielekea nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya nyumba yake ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa nguvu nyumbani kwake.
Mbwijo aliiambia mahakama kuwa, baada ya mshitakiwa kumwingiza ndani ya nyumba yake msichana huyo, alianza kumnyonya ulimi kwa nguvu huku akimtomasa sehemu za siri kwa vidole.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati akimfanyia uovu huo, mtoto huyo alikuwa akiomba msaada kwa kupiga kelele muda ambapo majirani walifika eneo la tukio na kumkuta mshitakiwa akiwa ameshaanza kumvuta mtoto huyo sketi yake ya shule.

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulileta mahakamani hapo mashahidi watatu na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.
Akijitetea, Lugendo aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile alichokieleza kuwa yeye ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote wawili ni walemavu, hivyo ana watu wengi wanaomtegemea.
Hata hivyo, Hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha kinyama na hatari kwani kina weza kumsababishia mtoto huyo ugonjwa wa ukimwi. Alimtia hatiani na kumwadhibu kifungo cha miaka kumi jela.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...