Wapatanishi wa kimataifa wamerejea kwenye mazungumzo na Iran kuhusu namna
ya kuzuwia mradi wa nuklia wa nchi hiyo.
Waakilishi wa Iran wanasema wameeleza kwa ufupi mapendekezo yao muhimu
kwenye mazungumzo hayo yanayofanwa Kazakhstan.
Lakini mwanabalozi mmoja kutoka mataifa ya magharibi alisema Iran
haikutoa jawabu thabiti kuhusu mapendekezo ya karibuni ya mataifa makuu pamoja
na Marekani, Urusi na Uingereza.
Mataifa hayo yanasema yatapunguza baadhi ya vikwazo vya kiuchumi dhidi
ya Iran, iwapo nchi hiyo itaacha sehemu fulani za mradi wake wa nuklia.
Mwandishi wa BBC kwenye mazungumzo hayo anasema inaonesha pande hizo
mbili kama hazifanyi mazungumzo kwa sababu maneno yao yanapishana.
No comments:
Post a Comment