Vichwa Vya Habari
Language
Saturday, 16 March 2013
HABARI MUHIMU: KENYATTA APATA MTIHANI WA KWANZA, BEI YA MAFUTA IMEPANDA KENYA
Tume ya Nishati imetangaza ongezeko la bei ya petroli kwa Sh4.12 na
kuibua hofu kwamba huenda kiwango cha mfumuko kikapanda tena.
Hii ni mara ya pili kwa bei kupanda baada ya kushuka kwa muda. Petroli
sasa itauzwa Sh117.69 kwa lita Nairobi.
Bei ya dizeli ilipanda kwa Sh1.17 hadi Sh107.37 kila lita jijini, nayo
mafuta taa yakapanda bei kwa Sh2.61 hadi Sh88.54 kwa lita.
Labels:
HABARI MUHIMU
HABARI MUHIMU: UYANYASAJI WA WANAWAKE KUENDELEA?
Labels:
HABARI MUHIMU,
MENGINEYO
HABARI MUHIMU: ZITTO NA CHEYO HAPAKALIKI
Hatimaye Bunge limetangaza mabadiliko ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za
Bunge zinazotarajiwa kuanza kukutana kuanzia Jumatatu ijayo, huku baadhi ya
vigogo wakiwekwa katika kamati moja na kufanya zoezi la kuchagua wenyeviti wa
kamati hizo kuwa gumu.
Uteuzi wa majina ya wajumbe hao unakuja mwezi mmoja tangu kumalizika kwa Mkutano wa 10 wa Bunge ambapo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza mabadiliko ya kamati hizo, huku akiifuta Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitafanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).
Labels:
HABARI MUHIMU
HABARI MUHIMU: ALIYEWAUNGUZA MIDOMO WATOTO WAKE MOROGORO KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Polisi mkoani Morogoro, wanamshikilia mkazi mmoja wa Ujenzi, mjini
Morogoro kwa tuhuma za kuwaunguza midomo, watoto wake wawili kwa madai kuwa
waliiba na kula karanga zake.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Faustine Shilogile, alisema tukio
hilo lilitokea mapema wiki hii na kwamba mmoja wa watoto hao ana umri wa miaka
kumi na mwingine, mitano.
Kamanda Shilogile alisema mtuhumiwa alikwishaachana na mama wa
watoto hao ambao kwa sasa amekuwa akiishi nao.
Alisema karanga hizo zilikuwa ni za biashara ya baba yao na kwamba
taarifa za tukio hilo, zilitolewa na walimu wa Shule ya Msingi Msamvu B ambako
watoto hao wanasoma.
Kamanda Shilogile alisema walipofikishwa katika kituo cha polisi na
kuchukuliwa maelezo, watoto hao walipelekwa hospitalini kwa matibabu na
kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Labels:
HABARI MUHIMU
HABARI MUHIMU: HIVI UNAJUA KUWA PAPA FRANCIS I ALIKUWA BAUNSA WA MLANGONI BAA? SOMA HAPA UYAJUE MAISHA YAKE
Papa Francis I aliteuliwa hivi karibuni kuliongoza kanisa hilo baada ya
Papa Benedict XVI kutangaza kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Enzi ya ujana wake aliwahi kufanya kazi mbalimbali ikiwamo ya mlinzi wa
mlangoni (baunsa) katika Bar, ili kujipatia fedha.
Papa Francis aliteuliwa hivi karibuni kuliongoza kanisa hilo baada ya
Papa Benedict XVI kutangaza kujiuzulu kwa sababu za kiafya.
Labels:
HABARI MUHIMU
HABARI MUHIMU: VYETI VYA WALIMU KUCHUNGUZWA KWA KINA
Wadau wa elimu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara,
wameshauri Serikali kufanya ukaguzi wa kina wa vyeti vya taaluma za walimu, ili
kubaini kama wanaovitumia ndiyo wamiliki wake halisi.
Hatua hiyo inatokana na vyeti hivyo kuonyesha ufaulu mzuri kwa
baadhi ya walimu wilayani hapa, lakini hawana uwezo wa kufundisha darasani.
Wakichangia maoni kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya elimu
wilayani hapa uliofanyika juzi, wadau hao walisema hali hiyo inaifanya shule
kuwa na idadi kubwa ya walimu, lakini hawana taaluma ya ualimu.
Walisema kwamba hali hiyo ndicho chanzo cha kushusha kwa taaluma
shule za msingi na sekondari.
Labels:
HABARI MUHIMU
Subscribe to:
Posts (Atom)








