Language

Wednesday, 24 April 2013

KENYATTA ATEUA MAWAZIRI WANNE WAPYA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne. 

 Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.

Tuesday, 23 April 2013

UMEISIKIA STORY KUHUSU RAMA DEE KUTUA NCHINI NA KUWABWAGA MACHIZI WAKE? YEYE MWENYEWE KAFUNGUKA KUHUSU HILO


UNATAKA KUTUMA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU TCU? SOMA HAPA UJUE JINSI YA KUJIUNGA


Unaweza kutumia Internet au Simu yako ya mkononi. Soma kwa makini maelekezo hayo muhimu kisha kuna link mwisho itakupeleka kwenye fomu za kujisajili baada ya kuwa umeelewa cha kufanya. 

Applications shall be made using one of the two ways, namely, Internet and SMS applications. Applicants should not submit their applications to TCU or NACTE by e-mail, fax, or deliver them in person. 
Application through Internet  10.1.1 Holders of Tanzanian certificates applying through the Internet should go through the
following steps: 

N.E.C.T.A WAMEPANDISHA KIWANGO CHA UFAULU KIDATO CHA NNE, ANGALIA MARKS MPYA ZITAKAZOTUMIKA SASA


HIVI NDIVYO BARCELONA ALIVYOPIGWA NA 4 NA BAYERN MUNICH, ANGALIA SUMMARY YA MECHI YOTE HAPA



RATIBA YA MECHI KUBWA ZA APRILI 23 KATIKA MASHINDANO MBALI MBALI DUNIANI


HABARI KUBWA ZA APRILI 22 NA 23 KWA UFUPI


Boston attack motive still unclear Monday, April 22, 2013 11:34:02 PM
The motive for the Boston Marathon bombing remains unclear, after prosecutors charged the surviving suspect in hospital.
Explosion at French embassy in Libya Tuesday, April 23, 2013 12:21:52 AM
A car bomb explodes outside the French embassy in the Libyan capital, Tripoli, wounding two guards and causing extensive damage, officials say.
Japan warns China on islands landing Tuesday, April 23, 2013 12:19:39 AM
Japan would respond with force if any attempt is made to land on disputed islands, PM Shinzo Abe warns, as eight Chinese ships sail in the area.

MAREKANI YASHINIKIZA MAZUNGUMZO YA AMANI MASHARIKI YA KATI

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry yuko mjini Brussels ambako anatarajiwa kukutana na mkuu wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso, na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov. 

Kerry mwishoni mwa wiki alifanya ziara katika Ukingo wa Magharibi katika juhudi za kushinikiza kuanzishwa tena mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina. Bruce Amani ana mengi zaidi
Akiwa mjini Istanbul hapo jana Jumapili, waziri huyo wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry alimtaka Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuchelewesha ziara yake katika Ukanda wa Gaza mnamo Mei 16 baada ya kuitembelea Ikulu ya Marekani, kwa sababu itahujumu juhudi za kuimarisha mahusiano baina ya Uturuki na Israel.

Monday, 22 April 2013

VAN PERSIE NA USHINDI WA 20 WA MANCHESTER UNITED

Manchester United imetwaa rasmi ubingwa wa 20 wa taji la ligi kuu soka nchini England kwa ushindi wa mabao matatu ya aina yake dhidi ya Aston Villa,Mabao yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ambaye sasa atakuwa akiongoza safu ya wafungaji kwa kufikisha mabao 24 huku Luis Suarez akifuatia akiwa na mabao 23.
Van Persie alifunga mabao yote matatu ndani ya dakika 31 za kipindi cha kwanza katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Traford na kuwafanya United kufikisha pointi tofauti ya 16 na waliokuwa mabingwa watetezi majirani zao Manchester City,huku wakiwa na michezo minne kibindoni.
Mkongwe Ryan Giggs alianza kwa kumtengenezea nafasi ya goli la kwanza Van Persie dakika mbili baada ya mchezo kuanza kabla ya Wayne Rooney kumpa nafasi nyingine nzuri Van Persie dakika ya 13 na kufunga moja kati ya mabao bora kabisa msimu huu kwa mguu wake wa kushoto na kufanya United kuwa mbele kwa mabao mawili ndani ya dakika 15 za kwanza za mchezo.

MANCHESTER UNITED KUTANGAZA UBINGWA LEO IWAPO ITASHINDA LEO DHIDI ASTON VILLA


Ligi kuu ya soka nchini England itaendelea tena jumatatu ya leo kwa mchezo mmoja kati ya Manchester United watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Old Traford kuwakaribisha Aston Villa.

Mchezo huo ambao Manchester United inahitaji ipate ushindi kujihakikisha ubingwa wa 20 wa ligi kuu soka nchini England na kuweka rekodi mpya ya kuwa timu iliyochukua taji hilo mara nyingi zaidi ya Liverpool ambayo ilikuwa inashikilia rekodi ya mataji 19.
United inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kulazimishwa sare ya 2-2 na West Ham United katika mchezo wa jumatano iliyopita. Aston Villa wao watashuka uwanjani kucheza mchezo huo usiku wa leo wakiwa kwenye harakati za kuepuka kushuka daraja la ligi kuu.
United katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa michezo miwili,wameshinda miwili na kutoka sare mmoja huku Aston Villa katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa mchezo mmoja na kushinda michezo mitatu na kutoka sare moja dhidi ya Fulham.
Huu utakuwa mchezo wa 34 kwa timu zote kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza msimu huu ambapo zitakuwa zimebakisha michezo mingine minne kumaliza ligi.
United wanaongoza ligi wakiwa na point 81 huku wakifuatiwa na watani zao wa wajadi Manchester City ambao walifungwa hapo jana jumapili na Tottenham kwa mabao 3-1,hivyo mchezo wa leo utaweza kuwafanya United wacheze kwa uhuru zaidi na kutaka kujipa matumaini ya kuwavua rasmi ubingwa majirani zao Manchester City. Aston Villa inayofundishwa na Paul Lambert inashika nafasi ya 17 wakiwa na point 34,pointi tatu zaidi ya Wigan wenye pointi 31 wakiwa kwenye nafasi ya 18 ambayo ni kwenye kundi la timu tatu za mwisho zilizoko kwenye hatihati ya kushuka daraja.
Aston Villa katika michezo 32 iliyopita waliyocheza na Manchester United wameshinda mchezo mmoja,hiyo ilikuwa mwaka 2009 mwezi disemba pale Gabby Agbonlahor alipofunga bao la kichwa kwenye uwanja wa Old Traford. Kwa upande wa United, wao katika michezo 34 iliyopita ya ligi kuu tangu mwaka 1995 wamepoteza mara moja tu dhidi ya Villa.
Wayne Rooney anatarajia kufikisha mchezo wake wa 400 akiwa na Manchester United huku akiwa ameifungia klabu yake mabao tisa ya ligi kuu dhidi ya Aston Villa ikiwa ni rekodi nzuri kwake kuifunga timu moja idadi kubwa ya magoli,akiwa amezifunga idadi hiyo hivyo timu za Bolton, Fulham and Newcastle.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...