Language

Friday, 26 April 2013

NO CAPTION!!!


UHURU KENYATTA ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelitangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa kiasi kikubwa limeundwa na sura ngeni na wengi wao ni wasomi waliobobea kwenye fani mbalimbali.
Katika majina 16 aliyopendekeza ambayo baadaye yatafanyiwa uchunguzi na Bunge kabla ya kuidhinishwa, Rais Kenyatta amezirejesha sura mbili ambazo zilizoeleka kwenye siasa za Kenya, ambao ni Najib Balala na Charity Ngilu.

NI LULU TENA! ABAMBWA AKIJIUZA COCO BEACH AKIJIUZA


HIZI NDIO HABARI KUBWA ZA JANA KAMA HUKUFANIKIWA KUZIPATA


Fears for hundreds missing in Dhaka Thursday, April 25, 2013 11:41:50 PM
Hundreds of Bangladeshis are still missing two days after a building collapsed near Dhaka, killing at least 273 people, local officials say.
'Many dead' in Russia hospital fire Thursday, April 25, 2013 10:21:44 PM
At least 38 people are feared to have been killed in a fire at a psychiatric hospital in the Moscow region, officials say.
Cancer 'threat' to Latin America Thursday, April 25, 2013 6:05:29 PM
Cancer is threatening to overwhelm Latin American countries, experts writing in Lancet Oncology warn.
No response from N Korea on talks Thursday, April 25, 2013 10:14:16 PM
North Korea has not responded to South Korea's calls for talks on resuming operations at the jointly-run Kaesong Industrial Complex, officials say.
Franz Joseph hair sold at auction Thursday, April 25, 2013 3:02:20 PM
A buyer pays 13,720 euros for a lock of hair belonging to the Austrian Emperor Franz Joseph in an auction in Vienna.

MAZITO YALIYOANDIKWA KATIKA BARUA MAALUM KWA DIAMOND NA MAMA YAKE


Mbeya region
P.O.BOX 0759209081
MBEYA

Dear diamond....
sina imani we ni mzima wa afya kutokana hasa na mambo unayofanya kiukweliii katika wasanii wakali mpaka kupitiliza hapa Tz wew ni mmoja wapo.. napenda sana vibonzo vyako hasa kile cha " nani amenuna nani amenuna eti nani amenuna" najua utakua umemalizia WEMA... katika kila shoo zako unazofanyaga mara nyingi huwa unataja kumheshim sana mama yako mzazi kutokana na malezi aliyokupa toka kipindi kile unauza MITUMBA.. lakini saiz unafanya mama wa watu aonekane alizaa toto zinzi ambalo kama limetumwa kuzini na kuumiza wanaume wenzie.. ivi unajua mke anauma kias gani hata kama wanajileta we ni mtu mzima ambaye unatakiwa kupembua mambo.... hasa kuhusu jambo la HILI MBURULA LENZIO UWOZO or SORRY I mean UWOYA.. unajua kabisa kaka yetu NDIKU ambaye anafanya kazi ngumu ya kukabana na wakina NSAJIGWA, FUSO uwanjani ili apate chochte cha kulisha family yake lakini wew bila huruma una ramba asali yake... ivi unajua mtoto wa uwoya "krish" atakopukua njiani kwenda shule wenzie watakua daily wakimuambia " mtoto wa kambo wa DOMO huyo' ivi dear diamond mbna unataka mama yako asipewe heshma sababu ya wew hujui ka unamfanya awe despsd infrnt of da pple...
najua hujaelewa coz elimu kwako ni tatizo utampigia wema akufafanulie ila usi mrecord coz anakusaidia ww.... au umea athirika unafanya kusambaza.. hawa wanawake wapo toka enzi za ma dinossaurs,,, mwambie penny akuambie MAANA ya dinossaurs.. huu mda unaoangaika na wanawake ungejiendeleza ata kielimu iyo 4m four itakufksha wap.. na wew mama diamond ivi huoni anachofanya mwanao unashindwa kumshauli au unataka uje kumwambia akishaanza kuharisha na kumvisha visepe.. ERIC SHIGONGO naomba ukiiona hii itupie kwenye ijumaa wikienda ili babu yangu wa ileje Ambaye hatumiii fb asome mana kila siku amekua akiipenda nyimbo ya mbagala bila kujua uovu wa aliyeimba kwa leo yatosha ila TACAIDS naamini itakutemblea diamond siku si nyingi kkupa matumizi sahihi ya ARV's

wako shabiki namba MOJA DUNIA NZIMA....... via mbele kuchungu

Thursday, 25 April 2013

TUKIO LA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KATIKA PICHA


MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA APRILI 25


UNAMFAHAMU ALIYEBUNI JINA LA TANZANIA? MSOME HAPA


HISTORIA ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kutaja jina la mtu maarufu aliyebuni jina la Tanzania ambaye kwa bahati mbaya au kwa makusudi hakumbukwi tena.


Tunaelezwa kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini nani kati yetu amekuwa akijiuliza jina la Tanzania lilivyopatikana na nani hasa alilibuni?
Wengi tunaambiwa kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibari na raia wengine wa nje lakini hawatajwi waziwazi na picha zao tukaziona.
Inaaminika kuwa mtu aliyebuni jina la Tanzania ni MOHAMMED IQBAL DAR, raia wa India ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshindana katika shindano la kubuni jina la nchi mpya baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana.
Mohammed alizaliwa mkoani Tanga miaka ya 1944; baba mzazi wa Mohammed alikuwa daktari huko mkoani Morogoro akiitwa Dk. T . A DAR aliyefika Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya msingi mkoani Morogoro katika Shule ya Msingi H. H D Agakhan ambayo kwa sasa ni mali ya serikali. Alijiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe alikosoma kidato cha kwanza hadi cha sita.

BRAZIL KUONGEZA NGUVU KATIKA KIKOSI DRC

Umoja wa Mataifa umemteua Generali mmoja raia wa Brazil ambaye anasifika kwa kudhibiti mtaa mmoja wa mabanda nchini Haiti kutokanamana na vurugu kuweza kuwaongoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 20,000, ikiwemo kikosi kipya cha wanajeshi kitakachopambana na waasi mashariki mwa nchi.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Umoja wa mataifa kukabidhi kikosi cha wanajeshi nguvu kuweza kupambana na waasi.
Generali Santos Cruz, aliambia BBC kuwa wanajeshi wake, watafunzwa namna watakavyo pambana na waasi bila kuwajeruhi raia na kuharibu mali nchini Congo.
"eneo tete zaidi siku hizi ni Mashariki mwa nchi,'' Cruz alimbia BBC
"niko tayari kukabiliana, na hali ngumu zaidi. Lengo kuu ni kuwaondolea hali ngumu wanayokabiliana nayo watu wa Congo.''

KURA ZA MAONI KUPIGWA JUU YA AMANI NCHINI MALI


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio linalopendekeza kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani nchini Mali.

Kikosi hicho chenye wanajeshi 12,600 kinajumuisha takriban wanajeshi 6,000 kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika ambazo tayari zina wanajeshi wao nchini humo.
Azimio hilo limependekezwa na Ufaransa ambayo iliingilia kati mzozo wa Mali mnamo mwezi Januari ili kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Mali mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya uchaguzi mkuu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...