Language

Tuesday 22 January 2013

HABARI: KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA MISHENI MASHARIKI LAWAKA MOTO

HALI si shwari tena katika Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki kutokana na Mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi na Mkutano Mkuu wa Jimbo (Sidodi), Mchungaji Clement Fumbo kujichukulia madaraka na kutangaza uongozi wake mpya.
Fumbo alitangaza uongozi huo juzi katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Tabata akieleza kuwa uongozi wa juu wa kanisa unamtambua kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kanisa katika jimbo hilo la Misheni.
Wakati hayo yakijiri sintofahamu imebakia kwa waumini kuwa hivi sasa waufuate uongozi upi wa mwenyekiti aliyesimamishwa na sinodi ama Makamu Mwenyekiti Sauli Kajura aliyepewa mamlaka ya kuliongoza jimbo hadi kipindi cha mkutano mkuu wa uchaguzi utakaofanyika mwaka 2014.
Kutangazwa kwa uongozi huo wa kanisa kumejiri wakati pia kesi ikiendelea katika Mahakama ya Kisutu ambapo Mchungaji Fumbo alifungua kesi ya kupinga uamuzi wa Sinodi akieleza kuwa hakuhusika na upotevu wa Sh 500m hali iliyosababisha avuliwe uongozi huo kupitia sinodi ya dharura.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...