Language

Saturday 16 March 2013

HABARI MUHIMU: ALIYEWAUNGUZA MIDOMO WATOTO WAKE MOROGORO KUFIKISHWA MAHAKAMANI


Polisi mkoani Morogoro, wanamshikilia mkazi mmoja wa Ujenzi, mjini Morogoro kwa tuhuma za kuwaunguza midomo, watoto wake wawili kwa madai kuwa waliiba  na kula  karanga zake.

Kamanda wa Polisi mkoani humo,  Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea mapema wiki hii na kwamba mmoja wa watoto hao ana umri wa miaka kumi na mwingine, mitano.
Kamanda Shilogile alisema mtuhumiwa  alikwishaachana na mama wa watoto hao ambao kwa sasa amekuwa akiishi nao.
Alisema karanga hizo zilikuwa ni za biashara ya baba yao na kwamba taarifa za tukio hilo, zilitolewa na walimu wa Shule ya Msingi Msamvu B ambako watoto hao wanasoma.
Kamanda Shilogile alisema walipofikishwa katika kituo cha polisi na kuchukuliwa maelezo, watoto hao  walipelekwa hospitalini kwa matibabu na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...