Language

Thursday 14 March 2013

HABARI MUHIMU: GAVANA ALIYEIBA FEDHA AACHIWA HURU NIGERIA

Vyombo vya sheria nchini Nigeria vimemsamehe gavana wa zamani Diepreye Alamieyeseigha aliyeshutumiwa kuiba mamilioni ya dola kutoka kwa serikali. Msamaha huo ulitolewa na baraza la serikali, linalojumuisha rais Goodluck Jonathan ambaye aliwahi kuhudumu chini ya bwana Diepreye.
Mwandishi wa BBC nchini humo amesema kuwa hatua hiyo, ambayo imepingwa vikali na wanaharakati dhidi ya ufisadi, inamaana kuwa bwana Diepreye ataruhusiwa kuwania wadhifa wa kisiasa.
Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Bayelsa ambaye alitiwa nguvuni nchini Uingereza mwaka wa 2005 alikwepa kifungo kwa kukimbilia nchini Nigeria akiwa amevaa mavazi ya kike.
Amehudumu siku mbili tu ya kifungo cha miaka miwili aliyohukumiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...