Language

Tuesday 5 March 2013

HABARI TOKA VENEZUELA: RAIS HUGO CHAVES AMEFARIKI DUNIA

Makamu wa Rais nchini Venezuela  ametangaza kifo cha Rais wa nchi hiyo Hayati Hugo Chaves aliyekutwa na mauti akiwa umri wa miaka 58 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kansa kwa muda mrefu.




Jumapili iliyopita kupitia hapahapa Bonmusic Blog nilikuhabarisha juu ya Rais Hugo Chaves kuwa hakuwa amefariki kama minong'ono mingi ilivyokuwa imeenea na badala yake alikuwa akiendelea kupata tiba nchini Cuba ambako alikuwepo kwa muda mrefu.
Paoja na kukanushwa kwa habari hizo na wanausalama wa Venezuela, bado minong'ono iliendelea kueleza kuwa Chaves alikuwa amekufa tayari lakini habari zilifichwa ili kuweka sawa hali ya kiusalama nchini humo mpaka leo hii Makamu wa Rais alipotangaza msiba huo mzito kwa wananchi na wafuasi wa kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...