Language

Friday 12 April 2013

DOLA MILIONI 158 KUTATUA KERO YA MAJI ARUSHA



Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Arusha, Injinia Ruthi Koya alisema kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha ndiko kutatatua tatizo la maji.

Alisema mamlaka hiyo haina kiasi hicho cha fedha kwa sasa bali inategemea ruzuku ama mkopo ili kuweza kumudu kutatua tatizo la maji linalozidi kulikabili jiji hilo, hasa baada ya kuongezewa maeneo kutoka wilayani Arumeru.
Injinia Koya alitaja maeneo ambayo hadi sasa hali ya upatikanaji maji si nzuri ni pamoja na Olasity, Kwa Mrombo, FFU na baadhi ya maeneo ya Mianzini ambapo jitihada zinafanywa kupunguza makali hayo.
Alifafanua kuwa baada ya mamlaka hiyo kuchimba kisima kirefu katika eneo la Sombetini, wanatarajia kuyasambaza maji hayo katika maeneo ya Olasity na Kwa Mrombo ambako kuna tabu kubwa ya maji.
Alisema uwezo wa mamlaka hiyo kwa sasa ni kuzalisha lita za ujazo milioni 45,000 kwa siku huku mahitaji halisi yanayotakiwa ni lita milioni 93,270 kwa siku hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kufikia malengo hayo.
Aliomba wananchi kumvumilia kwa kipindi cha miaka mitano kuweza kutatua changamoto hiyo ya upatikanaji maji safi na huduma ya uondoaji maji taka mjini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...