Language

Friday 12 April 2013

LIGI KUU YA VODACOM INAPIGWA TENA LEO KATIKA VIWANJA MBALI MBALI



www.facebook.com/bonmusicblogLigi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.
Ligi hiyo itaendelea kesho (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...