Language

Wednesday 3 April 2013

JUMA NATURE MWAMBA WA TEMEKE



Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano wa Wanaume Halisi na Wanaume Family wamemtunuku Juma Kassim ‘Nature’ kuwa Mfalme wa Temeke kutokana na jinsi walivyomkubali na kumwamini.
Mpambano huo ulioteka hisia za watu wengi, ulipigwa Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, jijini Dar ambapo mbali na umati mkubwa wa mashabiki hao kumshangilia Juma Nature na kundi lake, walionyesha kukubali onyesho la Wanaume Family walipokuwa jukwaani.
Umati wa mashabiki ulipiga mayowe ya furaha kuonyesha kuwa wamekubali zaidi onyesho la  Wanaume Family kuliko hata lile la Wanaume Halisi haswa walipokuwa wakitumbuiza nyimbo zao zinazopendwaukiwemo Dar Mpaka Moro, Mkono Mmoja,  pamoja na nyingine nyingi kali ambazo walinogesha zaidi walipokuwa wakirusha miguu hewani kwa mtindo wa ‘mapanga shaa’.

Baada ya kila kundi kupanda jukwaani kwa awamu mbili tofauti, jaji wa mpambano huo John Dilinga ‘DJ JD’ aliwataka mashabiki kumtaja Mfalme wa Temeke ambapo walijibu kwa pamoja;  “Nature”  hivyo kumfanya mkali huyo anayewakilisha kundi la Wanaume Halisi kuwa  Mfalme wa Temeke ingawa kwa namna moja au nyingine walikubali zaidi onyesho la Wanaume Family, lakini mapenzi yao yako kwa kinara huyo.
Mbali ya onesho kali la mpambano huo, mkongwe kwenye muziki wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na Inspector Haroun waliutumia vyema muda wa mapumziko ya mpambano huo kutumbuiza nyimbo zao zinazobamba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...