Takriban watu 27 wamefariki baada ya ardhi kuporomoka mjini Petropolis,
eneo la milimani kaskazini mwa Rio de Janeiro, Brazil, baada ya mvua kubwa
kunyesha.
Maporomoko hayo ya ardhi yaliukumba mji wa Petropolis baada ya mto
kufurika.
Kundi kutoka Brazilian National Force limetumwa eneoni ili kuwasaidia
waokoaji.
Kwa sasa mji huo uko katika hali ya tahadhari kwa sababu mvua zaidi
inategemewa. Shule zimefungwa na wakaazi wametahadhirishwa wabaki majumbani
mwao.
Wapoteza makao
Inakisiwa kwamba takriban watu 50 wamepoteza makao.
Eneo linalozunguka Petropolis lilikumbwa na maporomoko mnamo 2011
ambapo watu 900 walifariki.
Mwandishi wa BBC, Julia Carneiro aliyeko Rio, anasema kwamba ahadi toka
kwa vyombo vya dola kwamba watajenga mikakati ya kuzuia visa kama hivyo
hazijafua dafu.
No comments:
Post a Comment