Maafisa wa utawala nchini Afrika Kusini wanasema kuwa rais mstaafu Nelson
Mandela anaendelea vyema na matibabu baada ya kulazwa hospitalini kwa siku ya
pili akiwa na maradhi ya kifua.
Taarifa kutoka rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ilisema kuwa hali ya
Mandela inaendelea kuimarika na kwamba hata aliweza kula vyema kiamsha kinywa
chake.
Mapema leo Jacob Zuma, aliwahakikishia wananchi wa Afrika Kusini kuwa
rais mstaafu Nelson Mandela anatibiwa ugonjwa wa mapafu ambao umekuwa ukitokea
mara kwa mara.
Katika mahojiano na BBC , bwana Zuma alisema kuwa watu hawapaswi kuwa
na wasiwasi kwani Mandela anaendelea kupokea matibabu.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kabla ya Jumatano
usiku.
Alikuwa hospitalini kwa siku 18 mnamo mwezi Disemba, akipokea matibabu
ya mapafu na kibofu.
Katika taarifa yake iliyotolewa mapema, Zuma alisema kuwa Mandela
anaendelea kupokea matibabu.
No comments:
Post a Comment