Takriban watu watatu wamethibitishwa kufariki baada ya jengo lenye
ghorofa zaidi ya kumi kuporomoka mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Zaidi ya wengine arobaini wangali wamenaswa chini ya vifusi.
Shughuli ya ujenzi ilikuwa inaendelea kwenye jengo hilo wakati
lilipoporomoka katikati mwa mji wa Dar es Salaam.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe
kutaka msaada.
"nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia
mayowe,'' alisema shahidi mmoja.
Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na liliporomoka saa tatu
kasorobo asubuhi kwa saa za Afrika mashariki.
Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa
nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado
haujulikani.
No comments:
Post a Comment