Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule, a.k.a Profesa
Jay, amesema hajashangaa kujikuta katika orodha ya mwanzoni kabisa ya
wanamuziki wa heshima waliotajwa kushiriki tamasha lililoandaliwa na
mwanamuziki nguli kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone.

Katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na Mwananchi, Jay amesema
ukiachana na suala la muziki, yeye ni kama kaka wa wanamuziki kwa sasa.
Jay ambaye kwa sasa anasikika katika vituo vingi vya redio kupitia nyimbo
zake nyingi ukiwamo ule alioshirikishwa na Lady Jaydee wa Joto na Hasira,
anatajwa kuwa mwanamuziki aliyetia ushawishi wa hali ya juu kwa wasanii
wachanga kuanza muziki hapa nchini.
Onyesho hilo linatarajia pia kukusanya na wanamuziki kutoka Kenya, litafanyika
katika siku tatu mfululizo ambapo siku ya kwanza, itakuwa ni tarehe 26 Aprili,
katika viwanja vya mchezo wa rugby vya Kyandondo jijini Kampala, kisha Colline
Hotel siku itakayofuata katika Mkoa wa Mukono na litafunwa Entebe tarehe 28
katika fukwe za rResort Beach.
No comments:
Post a Comment