Language

Saturday, 30 March 2013

KIM JONG-UN AWEKA TAYARI MAKOMBORA YAKE



China na Urusi zimeelezea hofu ya kukithiri kwa mzozo katika rasi ya Korea na kutaka pande zote kujiondoa katika majibizano.

Hii inafuatia hatua ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuweka tayari makombora ya masafa marefu kukabiliana na tishio la mashambulio kutoka kambi za kijeshi za marekani na ndege zake za kivita.
Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amekashifu kile alichokitaja kama kuvuka mipaka kwa Korea Kaskazini.
Agizo la rais Kim Jong-un limetokana mazungumzo kujibu hatua ya ndege za kivita za marekani kuruka katika anga ya rasi ya Korea.
Alinukuliwa akisema kuwa muda umewadia wa kumaliza mgogoro na Marekani.
Korea Kaskazini imeghadhabishwa na hatua ya Umoja wa Matifa kuiwekea vikwazo vipya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...