WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda ameunda tume kuchunguza matokeo mabaya ya mtihani wa Kidato cha Nne mwaka
2012, Chadema kimesisitiza msimamo wake kwamba kitafanya maandamano kushinikiza
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na Naibu wake,
Philipo Mulugo wajiuzulu.
Vichwa Vya Habari
Language
Friday, 1 March 2013
HABARI MUHIMU: KIWANDA CHA GESI MTWARA CHAANZA KUJENGWA
HATIMAYE ujenzi wa kiwanda cha
kusafisha gesi kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam umeanza mkoani
Mtwara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya
China Petroleum and Technology Development Co-operation (CPTDC), ambao awali,
ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali kufikia mwafaka na
wananchi wa Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (Wilman
Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi
walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema Maswi.
HABARI MUHIMU: WANAUME MILIONI 2.8 KUTAHIRIWA MPAKA 2015
SERIKALI imejiwekea lengo la
kutahiri wanaume milioni 2.8 ifikapo mwaka 2015, baada ya kufanikiwa kuwatahiri
287,055 kati ya mwaka 2010 na 2012.
Hayo yamebainishwa katika taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya
tohara ya kitabibu kwa wanaume ilianzishwa mwaka 2010.
Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo
ilibainika kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Iligundulika kiwango cha juu cha
maambukizi ya VVU ambako kuna kiwango cha chini cha tohara kwa wanaume.
Mikoa hiyo ni ya Iringa, Njombe, Simiyu, Geita, Katavi, Mbeya, Rukwa,
HABARI MUHIMU: KONDOM FEKI ZINAZIDI KUSAMBAZA MAAMBUKIZI YA HIV/AIDS
WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku Uingereza mwaka jana
zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za gonjwa la ngono hatari
lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25 Uingereza, huku wataalamu wakionya
kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa
mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye vipele vipele ambazo
mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza iliingia katika msako mkali
kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi
18 iliyopita.
MICHEZO: BENITEZ OUT MEI MWAKA HUU
Rafael
Benitez, amesema kuwa atakihama klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja
uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Akiongea baada ya kuongoza
Chelsea kushinda klabu ya Middlesbrough kwa magoli mawili kwa bila katika mechi
ya raundi ya tano ya kuwania kombe la FA, kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile
aliwashutu mashabiki wa klabu hiyo.
Katika mahojiano na BBC, Benitez amesema
uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha
HABARI MUHIMU: OBAMA KUSHIRIKI UAPISHO WA RAIS MPYA WA KENYA
HABARI MUHIMU: HILI NDILO TAMKO LA MWAI KIBAKI KWA UCHAGUZI UJAO
MICHEZO: RYAN GIGS ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED MPAKA 2014
Ryan Giggs mwenye umri wa miaka 39,
amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu ya Manchester United.
Mchezaji huyo sasa atasalia na Manchester United, hadi juni
mwaka wa 2014, na kukamilisha msimu wake wa 23 kama mmoja wa wachezaji kumi na
mmoja wa kwanza wa Manchester United.Nahodha huyo wa zamani wa Scotland,
alicheza mechi yake ya kwanza na Manchester United tarehe mbili mwezi machi
mwaka wa 1991 na maefunga magoli 168 baada ya kucheza mechi
Subscribe to:
Posts (Atom)






