Vichwa Vya Habari
Language
Thursday, 28 March 2013
OBAMA: SHAME ON US IF WE'VE FORGOTTEN
President Obama, standing with families of victims of gun
violence, Thursday made an emotional appeal for Congress to act on gun control.
"Shame on us if we've forgotten," Obama said in the White
House East Room referring to the 26 children and adults killed by a gunman at Sandy Hook Elementary School in Newtown,
Conn., on Dec. 14.
"It's been barely 100 days since 20 innocent children and six
brave educators were taken from us by gun violence – including Grace McDonnell
and Lauren Rousseau and Jesse Lewis, whose families are here today," the
president said.
"I haven't forgotten those kids. Shame on us if we've
forgotten."
Also there was the mother of Hadiya Pendleton, the 15-year-old honor
student killed in January at a park less than a mile from Obama's home in
Chicago. The cheerleader had attended Obama's second inaugural in Washington.
Labels:
HABARI MUHIMU
SELENA GOMEZ AND JUSTIN BIEBER REUNITE AT HER HOUSE IN L.A.
Justin
Bieber stopped by Selena
Gomez's home in Encino, California, on Wednesday afternoon before heading
back out on tour.
The "As Long As You Love Me" singer -- who arrived with
security in a large black van around 3:30 p.m. -- was there for an hour. Gomez
was home at the time, as she was seen driving off shortly after her ex left the
property.
So were Bieber, 19, and Gomez, 20, attempting to work through their
relationship issues in hopes of a reconciliation?
"Definitely not," a source close to the actress emphatically
tells omg!. "She is not getting back together with him."
While promoting "Spring Breakers," Gomez made it clear she is
enjoying the single life, even joking with David
Letterman about making Bieber cry post-split.
"She's really happy right now, surrounding herself around good
friends," continues omg!'s source. "She's been working a lot and is
excited for everyone to hear her album … including Justin."
Interesting! Let the lyric analysis start now … or, rather, on April
14, when Gomez performs her new single "Come & Get It" at the MTV
Movie Awards.
Meanwhile, Bieber is resuming his "Believe" Tour and is set
to perform in Munich, Germany, tonight. Unfortunately his days off in L.A. this
week didn't exactly go as planned.
The "Beauty and a Beat" singer is being investigated for battery after allegedly spitting in his
neighbor's face after a verbal altercation on Tuesday morning. Sources close to
Bieber insist that
Labels:
BURUDANI
SASA NI AMINI NA LINAH TENA
Kama wewe ni mpenzi wa burudani na ni mfuatiliaji mzuri wa
muziki wa kizazi wa kizazi kipya hapa Tanzania basi ni lazima unawajua vizuri ESTELINA
Sanga ‘Linah’ na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’.
Wakali hao wamenaswa katika pozi jipya la kimahaba zaidi baada ya lile
busu lililoonekana katika jukwaa la fainali za EBSS mwaka jana walipokuwa
wakiutambulisha wimbo uitwao ‘Mtima Wangu’.
Picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa ndani ya gari huku mwanadafada akimbusu Amini, imedakwa juzikati katika mtandao wa BBM, ambapo wadau wanaotumia mtandao huo waliwapongeza kwa kurudiana.
Picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa ndani ya gari huku mwanadafada akimbusu Amini, imedakwa juzikati katika mtandao wa BBM, ambapo wadau wanaotumia mtandao huo waliwapongeza kwa kurudiana.
Baada ya mwandishi wetu kumtafuta Linah, alipopatikana alijibu kwa
kifupi kwamba hana tatizo na Amini hivyo yupo huru kwa lolote mbele yake na
wanafanya naye kazi kwa karibu.
Kwa upande wake Amini, alipoulizwa juu ya ishu hiyo alitiririka: “Linah ni mtu wangu hivyo sina ubaya naye kwa kila kitu hatujawahi kugombana wala kusutana picha zisiwashtue watu,” alisema Amini.
Kwa upande wake Amini, alipoulizwa juu ya ishu hiyo alitiririka: “Linah ni mtu wangu hivyo sina ubaya naye kwa kila kitu hatujawahi kugombana wala kusutana picha zisiwashtue watu,” alisema Amini.
Labels:
BURUDANI
KAMA UMESIKIA SAKATA LA MARINGO SABA KUNYWA SUMU BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE, MKASA WOTE UPO HAPA
MCHEKESHAJI wa Kundi la Mizegwe, Rashid Coster ‘Maringo Saba,’ anadaiwa
kumfumania mkewe anayefahamika kwa jina la mama Zai kisha kuamua kunywa sumu
ikisemekana kuwa alitaka kujiua kwa hasira.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kimenyetisha kuwa, Maringo Saba aliandaa mtego wa fumanizi baada ya kuhisi mkewe anamsaliti kwa rafiki yake anayefahamika kwa jina moja la Sam.
Chanzo hicho kilizidi kushuka na mistari kwamba, baada ya staa huyo kuandaa mtego, ulizaa matunda Jumatano ya Machi 20, mwaka huu ambapo alimfumania mkewe akijivinjari na jamaa.
Sosi huyo alizidi kubainisha kuwa, mke wa Maringo Saba alipoona mumewe amemjazia umati kwa fumanizi hilo, alitimua mbio kwa vile ilidaiwa Maringo Saba alitishia kumfanyia kitu mbaya.
“Ilikuwa vurumai, watu waliokusanyika kufanya fumanizi walimtembezea kichapo Sam kabla hajafanikiwa kuchoropoka kwenye himaya ya chumba hicho na kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mwananyamala CCM,” kilisema chanzo.
Chanzo kingine kilicho karibu na mchekeshaji huyo (jina lipo) kilidai kuwa, baada ya tukio hilo, Maringo Saba alikutwa chumbani kwake amezidiwa ndipo ndugu zake walipomkimbiza kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Labels:
BURUDANI
TIMBULO: SKENDO HAZIJACHANGIA KUNIONGEZEA UMAARUFU
Msanii wa bongofleva Timbulo amesema kuwa yeye si msanii ambaye amepata
umaarufu kutokana na skendo kuliko kazi anayofanya ya muziki.
Timbulo amesema kuwa watu wanaosema kuwa yeye anapendwa kutengeneza
skendo ili aandikwe kwenye magazeti wanakosea kwa kuwa angetaka kufanya hivyo
basi angekuwa anatengeneza stori nzuri na si za kumchafua.
Msanii huyo alisema kuwa hajawahi kufanya kitu kama hicho kabisa,
"kuna vitu vya kutengeneza lakini si kashfa ambayo inaweza kuwa kidonda
cha milele, ningekuwa nataka kutengeneza kashfa nzuri basi ni bora
ningetengeneza stori za uwongo kuwa nimeenda kutoa msaaada sehemu flani lakini
si kwa kujichafua jina langu".
Tangu atoke na wimbo wa kwanza 'Domo langu' mwaka 2011 msanii huyo
amekuwa akiandikwa kwenye magazeti kwa skendo kuliko kazi anazofanya.
Labels:
BURUDANI
MSHAHARA KIMA CHA CHINI KUTANGAZWA MWEZI APRILI
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema mwezi ujao wanatarajia
kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote.
Akizungumza jana wakati wa mkutano kuhusu sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa
Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), alisema kwa muda
mrefu kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote
kilikuwa hakijabadilishwa.
“Kwa muda mrefu tulikuwa hatujatangaza kima cha chini cha mshahara,
lakini nafurahi kuwajulisha tu kwamba mwezi ujao tutatangaza rasmi,”alisema
Kabaka.
Pia alitahadharisha kuhusu utitiri wa vyama katika sehemu moja ya kazi
kushauri waajiri wasiruhusu wafanyakazi waanzishe kwa sababu vitakosa nguvu ya
kujadiliana na mwajiri katika kufunga mikataba ya hiyari .
Waziri huyo alisema sekta ya hifadhi ya jamii ina idadi ndogo ya
wanachama waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ukilinganisha na idadi ya
nguvu kazi iliyopo ambayo ni milioni 22.
Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii,
Irene Isaka alisema hadi sasa michango katika mifuko hiyo imefikia Sh 1.4
trilioni na kwamba mafao yanayolipwa yamepanda kutoka Sh500 bilioni hadi
kufikia Sh 724 bilioni.
Labels:
HABARI MUHIMU
VIONGOZI WA DECI KUHUKUMIWA HIVI KARIBUNI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 10, mwaka huu inatarajia
kupanga siku ya hukumu ya kesi ya kuendesha na kusimamia mchezo wa
upatu inayowakabili vigogo wa Taasisi ya Deci Tanzania Ltd.
Hakimu Mkazi, Stuwart Sanga, jana alizitaka upande
zinazohusika katika kesi hiyo, kuwasilisha mahakamani hoja zao kama washtakiwa
wana hatia ama la.Alisema “hoja hizo zinapaswa kuwasilishwa Mei 10 na kwamba siku hiyo hiyo atapanga siku ya hukumu.”
Hatua hiyo imekuja baada ya vigogo wa Deci, kumaliza kutoa utetezi wao kuhusu mashtaka mawili yanayowakabili.
Mashtaka hayo ni pamoja na kuendesha mradi wa upatu kinyume na sheria
za taasisi za fedha na kuendesha mradi huo bila kibali.
Julai 17, mwaka jana mahakama hiyo, iliwaona washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu na kuwataka kujitetea baada ya mashahidi 16 wa upande wa mashtaka, kutoa ushahidi wao.
Julai 17, mwaka jana mahakama hiyo, iliwaona washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu na kuwataka kujitetea baada ya mashahidi 16 wa upande wa mashtaka, kutoa ushahidi wao.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya mwaka 2007 na Machi 2009,
washtakiwa walikuwa wanachukua amana za watu bila ya kibali.
Labels:
HABARI MUHIMU
Subscribe to:
Posts (Atom)





