Language

Saturday, 13 April 2013

GLOBAL PUBLISHERS WAFICHUA DANGURO LA WASANII



Kampeni ya Fichua Maovu inayoendeshwa na Global Publishers inazidi kuibua mazito! Safari hii imefanikiwa kunasa danguro la ufuska linalodaiwa kutumia na wasanii chipukizi wa muziki na filamu za Kibongo ambalo ni zaidi ya yale yaliyotendeka enzi za Sodoma kabla ya dunia kuangamia, Risasi Jumamosi lina ripoti ya kushtua.

Kwa muda mrefu gazeti hili lilipokea malalamiko ya majirani katika nyumba moja iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam kuwa kuna danguro linalotumiwa na mabinti chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya kuchuuza miili yao kwa wanaume huku baadhi wakiwa ni wasanii chipukizi wa filamu na muziki wanaohangaika kutoka kisanaa.

AFRICAN LYON NA HOMA YA KUSHUKA DARAJA



Kocha wa African Lyon, Charles Otieno amesema kwa sasa wanaomba Toto African, Polisi Morogoro wapoteze michezo yao ili wasalimike na janga la kushuka daraja.
 
Kocha huyo alikiri hawana njia mbadala ya kukwepa janga la kushuka daraja kama si kuomba dua mbaya kwa Toto na Polisi tu kwa sasa.
“Siwezi kusema tumeshuka, bado tunamichezo mitatu mkononi endapo tutashinda uwezekano ni mkubwa wa kuendelea kubaki, hakuna njia ya kutubakiza zaidi ya Polisi na Toto kupoteza mechi zao ili sisi tuweze kupata nafasi kinyume na hapo ni lazima tutashuka tu”alisisitiza kocha huyo.
Lyon imebakiza mechi dhidi ya JKT Ruvu, Mtibwa Sugar pamoja na Mgambo JKT. (Jessca Nangawe)Text inakuja hapa.

BARCELONA KUKUTANA NA REAL MADRID KATIKA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA PALE WEMBLEY?



Barcelona na Real Madrid zinaweza kukutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley, London Mei mwaka huu baada ya ratiba ya mechi za hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo iliyotolewa jana mchana kuzitenganisha.
Barcelona wamepangwa kucheza na Bayern Munich, wakati Real Madrid watacheza na Borussia Dortmund.
Mechi za kwanza hizo zitachezwa kati ya Aprili 23, na 24 kisha marudiano kati ya Aprili 30 na Mei. 1. Katika Ligi ya Europa, Chelsea watasafiri kwenda Uswisi kucheza na Basel Aprili 25, huku Fenerbahce wakiikabili Benfica. Mechi za marudiano zitachezwa Mei 2.
Chelsea ni timu pekee ya England iliyobaki kwenye mashindano ya Klabu Ulaya baada ya kusonga mbele kufuatia kuitoa Rubin Kazan ya Russia.
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, ratiba iliyotolewa jana mjini, Nyon, Uswisi, iliepusha timu Ujerumani kukutaka kwenye hatua ya nusu fainali, vilevile timu za Hispania kwenye hatua hiyo.

UMEME WAKATIKA NUSU SAA BAADA YA MITAMBO KUZINDULIWA ZANZIBAR



Huduma za umeme katika Mji wa Zanzibar, jana zilikatika kwa zaidi ya nusu saa baada ya kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa umeme  kutoka Tanzania Bara.

Uzinduzi wa mradi huo, ulifanywa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, katika  Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Sherehe za uzinduzi wa mradi huo, zilihudhuriwa pia na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Hata hivyo muda mfupi baada ya shughuli hizo, huduma za umeme katika Mji wa Zanzibar, zilikatika  kuanzia saa 9 mchana na kudumu kwa zaidi ya nusu saa.
Meneja wa Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco), Mbarouk Hassan, alithibitisha kuwa huduma zilikatika na kwamba tatizo lilikuwa  Tanzania Bara.

UBADHIRIFU WA PESA ZA UMMA NCHINI TANZANIA



Maoni mbalimbali yanaendelea kutolewa nchini Tanzania juu ya ripoti ya mdhibiti mkuu na mkaguzi wa hesabu za serikali nchini humo, iliyomulika kiwango kikubwa cha ubadhirifu wa fedha za umma katika serikali hiyo.
 Ripoti hiyo imeaziangazia sekta au idara ya ujenzi, nishati na madini kuwa miongoni mwa idara zinazokuwa na ubadirifu wa fedha za umma.
Hata hivyo swali linaloulizwa ni je tatizo liko wapi kiasi ya kuwapo ubadhirifu mkubwa wa mara kwa mara katika fedha za umma?  Amina Abubakar amezungumza na Profesa Ibrahim Lipumba ni mtaalamu bingwa wa uchumi nchini Tanzania.Kusiikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

WAKIMBIZI MALI WAPO HATARINI, VIFO VYA WATOTO VYAZIDI KUONGEZEKA



Wakimbizi 74 elfu wa Mali wamekwama katika jangwa la Mauritania wakikumbwa na ukosefu wa maji na idadi ya vifo vya watoto ikizidi kuongezeka,linasema shirika la madaktari wasiokuwa na Mipaka-Medecins Sans Frontiere. 

Mzozo wa Mali umepelekea zaidi ya watu laki mbili na 70 elfu kuyapa kisogo maskani yao na kuranda randa ndani nchini huku wengine zaidi ya laki moja na 70 elfu wakikimbilia katika nchi jirani na hasa Burkinafasso,Mauritania na Niger.
Katika jangwa la Mauritania ambako hali ya hewa inapindukia nyuzi joto 50 kivulini, kambi ya wakimbizi ya Mbera inawapokea watu 74 elfu "walionasa jangwani" - kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Madaktari Wasiokua na Mipaka-Medecins Sans Frontièren-MSF.Watu hao wamekimbia mapigano,chuki za kikabila,ukosefu wa chakula na kuvurugika mfumo wa huduma za jamii.

MBUNGE ALLY KEISSY ATAKA BANGI IHALALISHWE TANZANIA



Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), jana aliwavunja mbavu wabunge baada ya kuitaka Serikali kutoa tamko la kuruhusu bangi kuwa zao halali la biashara kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Keissy ambaye amezoeleka bungeni kama mzee wa kulipua mabomu, alitoa kauli hiyo kupitia swali lake la nyongeza ambapo alisema zao la tumbaku nchini, halina maana kwa sasa zaidi ya bangi.
“Mimi naona hakuna sababu ya kuendelea kusimamia mazao ambayo hata dunia nzima wanayakataa kwa sababu yana ugonjwa wa kansa, leo Serikali itoe tamko ni lini itaruhusu zao la bangi kulimwa kama zao la biashara ili wananchi walime kwa uhuru,” aliuliza Keissy.
Alisema kuna faida kubwa katika kulima bangi kuliko kuendelea kulima zao ambalo watu wengine duniani wameliona kuwa halifai.
Katika swali lake la msingi, Mbunge wa Mpanda Vijijini, Selemani Kakoso (CCM), alitaka kujua ni lini zao la tumbaku litaingizwa kwenye ruzuku ya Serikali ili kupunguza gharama za pembejeo kwa wakulima wa zao hilo.

PANYA WANAOTAMBUA MABOMU WAFANYIWA MAJARIBIO MOROGORO



Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.

POLISI WAUA MAHABUSU MBEYA



Polisi mkoani Mbeya wanatuhumiwa kumshushia kipigo Barnabas Kahemele akiwa mahabusu na kusababisha kifo chake.
 
Kufuatia tukio hilo, ndugu wa marehemu Kahemele wamegoma kuuchukua mwili wa marehemu huyo uliohifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya wakidai kwamba mazingira yanaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kipigo cha polisi baada ya kumkamata.
Inadaiwa kuwa marehemu na wenzake wawili walikamatwa usiku ya Jumatano wiki hii, baada ya askari hao kufika nyumbani kwa marehemu, eneo la Uyole ya Kati. Mke wa marehemu Sara Muhwanji, alidai kuwa wakiwa wamelala walisikia mtu akigonga hodi na ndipo alipoamka na kutoka sebuleni.
“Nilitoka sebuleni na kuuliza nani anayegonga, ndipo nikasikia sauti ya mtu anasema kuwa mimi Mhagama, huyo ni jirani yetu pale nyumbani. Lakini sikufungua mlango na nikaenda kumwamsha

SASA MIPAKA YA SUDAN YA KUSINI KUFUNGULIWA



Rais Omar al-Bashir wa Sudan, katika ziara yake ya kwanza mjini Juba tangu nchi ya Sudan ya Kusini kuwa huru mwaka 2011, ametangaza mipaka kati ya nchi hizo mbili kufunguliwa.
Akizungumza akiwa na rais mwenzake, Salva Kiir, Bw Bashir alitaka pia mataifa hayo mawili kudumisha amani, na kuimarisha uhusiano wa kawaida tena.
Hali ya uhasama iliongezeka kati ya mataifa hayo mawili mwaka jana, huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka vita.
Uhasama huo umepungua, lakini tofauti kuhusiana na mafuta na ardhi bado upo kati ya nchi hizo mbili.
"Nimewaamuru maafisa wa serikali ya Sudan chama cha maslahi ya raia kushirikiana na ndugu zao katika Jamhuri ya Sudan ya Kusini", Bw Bashir alieleza katika hotuba yake katika mji mkuu wa Sudan ya Kusini, Juba.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...