Language

Tuesday 19 March 2013

BURUDANI: DULLAYO KALIZWA BODABODA YAKE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dullayo ameibiwa pikipiki yake (bodaboda) ambayo ilikuwa ikimuongezea kipato.

Huo umekuwa ni muendelezo wa matukio ya wizi ambao umekuwa ukimuandama mjanja huyo kwani ni piki piki yake ya pili kuibiwa.
Dullayo ameeleza kuwa alikuwa na pikipiki hiyo usiku wa kuamkia jana alikwenda kuipaki pikipiki hiyo eneo ambalo huwa anailaza kila siku lakini hakukuwa na nafasi hivyo akamkabidhi mlinzi wa eneo hilo.

Asubuhi alipoifuata hakuikuta na taarifa alizopewa ni kwamba mlinzi huyo ndie aliondoka nayo.

Tayari mlinzi anayetuhumiwa kuhusika katika wizi huo anashikiliwa na polisi lakini pikipiki pado haijapatikana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...