Language

Tuesday 19 March 2013

HABARI MPYA: UHURU KENYATTA AIFUKUZA KESI YAKE MAHAKAMA YA ICC


Wanasheria wa rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, wameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, kumfutia mashitaka yanayomkabili mbele ya mahakama hiyo.


Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Kikao maalum cha mahakama hiyo kimefanyika wiki moja baada ya mashitaka dhidi ya mshtakiwa-mwenza, Francis Muthaura, kutupiliwa mbali na mahakama ya ICC.
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuachiwa kwa Muthaura, pia kunafuta mashitaka dhidi ya Kenyatta, lakini mwendesha mashitaka wa ICC amesema ana ushahidi zaidi dhidi ya Uhuru Kenyatta.
Kesi dhidi ya Bwana Kenyatta, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu, na kutangazwa rais mteule baada ya kupata asilimia kidogo juu ya 50%, imepangwa kuanza kusikilizwa mwezi Julai.
Baada ya matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka 2007 - wakati Bwana Raila Odinga aliposhindwa dhidi ya Rais wa sasa Mwai Kibaki, zaidi ya watu 1,000 waliuawa na wengine 600,000 kuachwa bila makaazi.
Bwana Kenyatta, mtoto wa mwasisi wa taifa la Kenya, Jomo Kenyatta anatuhumiwa kupanga mashambulio dhidi ya makundi ya kikabila yaliyokuwa yakimuunga mkono Bwana Odinga kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...