Language

Thursday 11 April 2013

ALICHOKISEMA ZE BATO WA HIGH LIFE MUSIC KUHUSIANA NA BONGO FLAVA HIKI HAPA



Kawaida tumezoea kusikia  speech  mbali mbali toka kwa wasanii mbali mbali wa muziki hususan muziki wa Bongo Flava, lakini speech hii toka kwa msanii anaye kuja kasi katika game ya Bongo flava toka lebel ya High Life Music  Ze Bato ‘B 16’ kwangu naona katoa kitu kipya sana.

Akizungumza na BonMusic Blog katika Exclusive interview Ze Bato amesema kuwa “mimi kama msanii wa bongo flava ugumu katika muziki huu nahisi ni uelewa wa mashabiki na kukariri kuwa mtu fulani ndiye tunaye amini ni mkali lakini kumbe kuna watu wengi ambao ndo first time  kusikika katika masikio yao, ni wakali isipokua imani inakosekana. Lakini ujio mpya unatofauti kuliko tunavyoelewa japo yaliopo tunayaamini”
Pia  alimalizia kwa kusema haya..” napenda kuwashukuru mashabiki wangu, radio na blogs kwa kunipa mchango wenu mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki High Life Music Ameen”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...