Language

Thursday 11 April 2013

WATOTO NDIO WANAONGOZA KWA KUBAKWA NA KUDHALILISHWA KINGONO



Watoto ni wahanga wakubwa wa udhalilishaji wa kingono katika maeneo ya mizozo, linalalamika shirika la Uingereza, Save the Children na kuutaja utovu huo kuwa 'maovu makubwa na ya kutisha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo lisilomilikiwa na serikali, Save The Children, iliyochapishwa jana mjini London, zaidi ya asilimia 70 ya wahanga wa ubakaji katika nchi zilizoathirika zaidi na vita, mfano wa Liberia au Sierra Leone, ni watoto.
Uchunguzi uliofanywa umebainisha kwamba watoto wenye umri wa miaka miwili waliangukia mhanga wa visa vya kinyama vya maprofesa, wakuu wa kidini na wanajeshi waliopelekwa kwa ajili ya kutumikia harakati za kusimamia amani. Uchunguzi huo unazungumzia pia kuhusu vifo vya watoto walioangukia mhanga wa ubakaji au kudhalilishwa kingono na makundi ya wanajeshi.

"Inashtusha kuona idadi ya watoto walioangukia mhanga wa visa vya udhalilishaji wa kingono katika maeneo ya mizozo, ikifikia kiwango cha kutisha kama hicho," amesema Justin Forsyth, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la Save The Children. "Visa vya kuwadhalilisha watoto kingono ni mojawapo ya ushenzi mkubwa na uliofichika wa vita," ameshadidia mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...