Language

Thursday 11 April 2013

G8 WAILAANI KOREA



Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa manane yaliyoendelea zaidi kiviwanda wameungana kuilaani Korea Kaskazini, na kuitaka nchi hiyo kukomesha mara moja kutoa vitisho vya kivita
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Wester Welle, amesema katika siku ya pili ya mkutano wa mawaziri hao unaoendelea jijini London, Uingereza, kuwa mataifa yote ya G8 yanaaminini kuwa kuongezeka kwa matamshi hayo ya kuchochea vita kutoka kwa Korea Kaskazini lazima kusitishwe.
"Suala la kwa nini matamshi hayo ya kuchochea vita yanaongezeka – ingawa ni muhimu, lakini halina uzito mkubwa. Muhimu zaidi ni kwamba matamshi hayo hayapelekei kuripuka kwa vita. Na ndio maana ni muhimu sasa kuona jumuiya ya kimataifa ikiwajibika na kuzungumza kwa sauti moja.
Siyo pekee nchi za magharibi zinazobidi kuwa na msimamo mmoja, bali pia China na Urusi. Maoni yangu ni kwamba nchi hizi mbili pia zingependelea hivyo," alisema Wester Welle.
Korea kaskazini imetoa vitisho dhidi ya Korea Kusini, Japan na Marekani na inaonekana kujiandaa kufanya majaribio kadhaa ya makombora ambayo wadadisi wanasema huenda ikayafanya kwa wakati mmoja. Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, William Hague, alisema nchi iko njia panda hivi sasa, na inaweza kuishia kuwa taifa lililosambaratika na kutengwa, iwapo itashindwa kushiriki mazungumzo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...