Language

Friday 25 January 2013

HABARI: SITTA KUGOMBEA URAIS 2015

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015, iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati huo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa
Bunge.
Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... “Sina sababu za kuanza kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa watu sasa,” alisema Sitta.
Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi wa kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...